Salaam Ankal,

Naomba msaada kwa wahusika wa usafirishaji wa Qatar wanipatie begi langu. Nilisafiri kutoka Dar kuja Sweden kupitia Doha kwa kutumia Qatar, tarehe 2 August 2012. Nilikabidhi mizigo miwili ya mabegi pale Dar airport kwa kufuata utaratibu wote uliowekwa. 

Kwa bahati mbaya, nilipofika Sweden nimepata begi moja tu. Nikawauliza watumishi wa Qatar (Aralanda ), wakasema begi langu lingine limechelewa kufika , ila nisubiri ndege ya kesho yake. Walinihakikishia hilo kwa kunionyesha orosha ya mabegi yaliyochelewa kufika na langu lilikuwa miongoni mwa hayo mabegi.

Nimekuwa nafuatilia begi langu kwa muda wa wiki mbili sasa bila ya mafanikio yoyote.

Napata usumbufu, mateso , huzuni , majonzi na mipango yangu imekwama kwa upotevu wa begi langu. Kwa hilo, na kosa imani na usafiri wa Qatar . Inaonyesha watumishi wake sio waaminifu na wazembe katika kuhakikisha usalama wa mizigo ya abiria wao.

Nawaomba watu wa Qatar wanipatie begi langu haraka iwezekanavyo.

Jina: KHAMISI/
TICKET NUMBER: 1572308878339
TAG NUMBER: QR001413

Wanaweza wasiliana nami kwa simu number +46727871935

Mdau Khamisi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Sasa kakangu hamisi hao qatar wanafahamu kiswahili tutakusaidiaje mi ushauri uendelee kuwasiliana nao mpaka upate begi lako lakini ukituandikia humu hatukuelewi haya pole mdau

    ReplyDelete
  2. Sasa kakangu hamisi hao qatar wanafahamu kiswahili tutakusaidiaje mi ushauri uendelee kuwasiliana nao mpaka upate begi lako lakini ukituandikia humu hatukuelewi haya pole mdau

    ReplyDelete
  3. QATAR sio watu wazuri hata kidogo. Wana usumbufu mwingi sana kuanzia pale ofisini kwao hadi kule airport. Mimi wanachoniudhi ni tabia yao ya kuficha baadhi ya taarifa wakati wa kukata ticketi halafu siku ya kuondoka wanakung'angania pale airport ili uwape chochote. Vinginevyo wanakufutia safari yako.

    ReplyDelete

  4. SASA HILO NALO LA KULETA HAPA? NI SUALA LA KUFUATILIA HILO NI JAMBO LA KIMTAIFA MASHIRIKA YOTE MAKUBWA YA NDEGE YANAKUTANA NA SUALA HILO

    ReplyDelete
  5. Hii airline sio nzuri, ina ubaguzi hasa kwa waafrika. Nilienda Sweden na Qatar, nimeapa sitaitumia tena.

    ReplyDelete
  6. Mimi nilisumbuliwa hivyo mwaka juzi, bahati nzuri nililipata begi baada ya wiki, tangu hapo niliamua kuachana Kabisa na Qatar airways, ni afadhali nilipe zaidi KLM lakini niwe na Amani na safari yangu.

    ReplyDelete
  7. Tunashukuru kwa kutujulisha kuwa Qatar airways kuna uhuni. Kamwe sitapanda ndege yenye mambo ya ajabu kiasi hicho. Mzigo inafaurishwa kama kwenye basi la abiria halafu hawapo makini. Pole mdau.

    ReplyDelete
  8. Naona hili limekuwa tatizo kwa mashirika ya Ndege.Mimi nina Mwezi sijapata begi langu.Nilisafikri na KQ(Kenya Airways) tangu tarehe 21/7/2012 hadi sasa sijapata bag langu.Tuwe wapole tu, hata tukigombana nao haisaidii.

    ReplyDelete
  9. Qatar si ndege nzuri hata kidogo, niliwahi kusafiri nayo kwenda London, nilifika begi langu limefunguliwa kwenye zipu, na jinsi walivofungua ni kwamba begi haliwezi kutumika tena ! wapuuzi sana hawa watu, ndege inayokuja Tanzania ni chafu chafu chafu ! halafu kwa ubaguzi ndio usiseme! niliignia wakatuweka sets tofauti na mtoto wangu wa miaka 5, baada ya seat yangu kuwapa wazungu wawili mke na mume mie nikasimama pale pale nikawaambia sikai sehemu mbali na mtoto wangu sasa mtaamua mfanye nini mpaka akatokea mtu alikuwa na mwenzake anatoka nchi moja akajitolea kuja kukaa kwenye seat yangu namie nikae na mwanangu, haikuishia hapo! wakati najaza landing zard ya Tz, mie sijamuangalia yule mdada anatoa vitambaa vya kujifutia basi akaweza kwenye meza nikamuita, nikamwambia mbona umeweka hapa? wengine unawapa mkononi au TUMELIPA NAULI TOFAUTI??? akachukuwa na kuniletea kingine yaani NILIAPA SISAFIRI TENA NA HII NDEGE !

    ReplyDelete
  10. Yalinikuta na Oman Air pale Muscat, jamaa wabaguzi tena wanajua kiswahili. Wazungu wanawashughulikia vizuri hata masuali hawawaulizi nilipofika mimi anaanza kuniuliza unakwenda UK kufanyanya nini mara apekue pasi yangu mara kaa kule mara hivi. Sipandi tena ndege yao hata kama inapita Zanzibar. Waliniweka masaa zaidi ya 12 bila hata maji. Pesa lao bomu kweli kweli chip kuku sawa na £15. Kila kitu ghali.

    ReplyDelete
  11. fuatilia na Airline kama hawataki nenda IATA. Kutokan na maoni inaonekana hii Airline sio nzuri lakini inajulikana kama 5 star airline manake inashinda tuzo nyingi

    ReplyDelete
  12. mtu (kampuni pia ni mtu/watu) aachi asli yake yaani culture. Bora utafute mashiriki yanayojali watu wa asli mbalimbali.

    ReplyDelete
  13. Suala la mizigo si la Qatar peke yake. Tatizo hilo linajitokeza kwenye ndege nyingi sana. Hata mnaosema mtasafiri na KLM, rafiki yangu alipotelewa na begi lake mwaka jana, alikuja kulipata baada ya wiki mbili. Mimi juzi tu sikuweza kupata begi langu moja, lakini nimelipata leo. Nilisafiri na Turkish Airlines. Muhimu ujue njia zinazopaswa kufuata katika kudai BEGI lako. Kulalamika hapa kwenye mtandao ambao hausomwi na maafisa wa Qatar ni USHAMBA. Labda kama ungekuwa unahitaji msaada kutoka kwa wenye uelewa hapo sawa. Lakini ukiingia kwenye 'site' yao, utaona nini unatakiwa ufanye. Ikitokea mzigo ukapotea kabisa, unalipwa na BIMA. Fuatilia, uache uvivu.

    ReplyDelete
  14. Waarabu tangu lini wakawa wastaarabu?. Do everything you can to avoid Arabs. They are uncivilized and uncultured.

    ReplyDelete
  15. Mabegi mengine hucheleweshwa kwaajili ya mamabo ya usalama, kwani na sisi wabantu .......

    ReplyDelete
  16. Ndugu zangu Watanzania!
    Kuhusu swala la mabegi kuchelewa au kufunguliwa hayo yanatokea kwenye mashirika yote.Kuchelewa ni kwasababu mfumo wa sasa wa usalama wa usafiri ni lazima mabegi au mizigo ikaguliwe tena na hata kama hawana access wanafungua na kuharibu sanduku au begi na mashirika hayalipi siku hizi tangu mtindo huo uanze na hii imeazishwa baada ya septemba 11.nimesafiri mara nyingi na hii hutokea mara nyingi na has got nothing to do with airlines but something to do with Travel security agencies za nchi mbali mbali.Hawa QATAR Nimeshasafiri nao mara kadhaa si wabaya hivyo.Mwaka huu nilisafiri nao niligombana nao pale airport nimetoa kila Document baada ya kila kitu kuwa sawa jamaa hataki kuniruhusu kijana mbongo anayekagua document ati mpaka nimjibu nilikuwa nafanya nini Tanzania nikamwambia mimi ni mtanzania wewe unaniuliza nilikuwa nafanya nini nyumbani kwasababu tu nafanyakazi nje tena ninarudi kazini?labda ungeniuliza naenda kufanya nini niendako sasa wewe umekuwa uhamiaji au TISS labda wanamashaka na nyendo zangu na nimekuja kufanya nini TZ sasa wewe huna haki ya kuniuliza nyumbani nchini mwangu nimekuja kufanya nini.Akaacha kunihudumia na mimi nikawakomalia kwamba hapa ni nyumbani haja ya kukueleza nilikuwa nafanya nini kwangu haipo na nikawagomea ,shughuli za kasimama na kumuita mdada mmoja ambaye ni supervisor wakaleta kejeli lkn siku ya siku waliniachia na nikaondoka.Huo ndiyo ujinga wa hiyo Airline wanapokagua documents. hapo sasa napata picha kuna mdau anasema wanaomba chochote kwangu walikwaa kisiki huwezi kuniuliza kama mtanzania nilikuwa nafanya Tanzania na iwe ni moja ya kigezo cha kuniruhusu mimi kupanda ndege.

    ReplyDelete
  17. We are becoming so dependent on the internet we cant even think for ourselves. This is rather a personal issue but since you brought it here, we'll help you think.
    As said above, delayed/missing luggage problems is not on Qatar only, as a frequent traveler, I have experienced this one too many times but I don't boycott any airline.
    Next time when you travel and have two bags, try to split your items between the bags, for instance dont put all shirts in one bag and all trousers in the other, that way you don't get stuck with missing items in a case where you get one of the two bags. As a rule of thumb, all important items like documents, laptops, house/car keys, money etc that you feel like you will need to use immediately when you get to your destination should be carried in your carry on luggage. All other things can be purchased if you really need them while they are delayed.

    ReplyDelete
  18. Huyo jamaa anayetukana waarabu kuwa sio civilized inahusiana nini civilazation na biashara ya usafiri wa anga?kwanza nataka aelewe kampuni nyingi za ndege duniani zina wafanyakazi toka nchi mbalimbali na zinaongozwa kwa utaratibu wa kikampuni na sio Ukabila kama jamaa anavyoropoka.Ubovu Watanzania siku zote hatuishi kulalamika hata kwa mambo madogomadogo ambayo mtu unaweza kuyamaliza mwenyewe au kwa msaada wa wengine.sasa wewe uliyekuwa civilized mbona huna ndege yako?

    ReplyDelete
  19. Wewe unayesema ulikaa Muscat masaa 12 inaonyesha ni mara yako ya kwanza kusafiri,Popote pale ukienda kukata ticket ya ndege lazima uulize transit hours itakuwa masaa mangapi na kama Airline inatoa Hotel Accomodation kwa muda huo utakaokaa Airport ukingojea ndege yako ya kuunganisha au kama utataka kulipia Hotel ili iwe included kwenye ticket yako pia elewa siku hizi airline nyingi unaweza kuchagua chakula unachota upewe kwenye ndege,nashangaa unapolalamika kuwa uliuziwa chips kuku kwa pound 15 au unataka kutudanganya kuwa London Heathrow chakula ni rahisi ili tukuamini.Brother ukiwa unasafiri kabla ya kukata ticket unahitaji ujue kila kitu,elewa kanuni ya IATA inakwambia transit ikizidi masaa 8 lazima upewe Hotel je wewe kabla ya kukata ticket uliulizia hayo?

    ReplyDelete
  20. Je huyo jamaa anayesema Waarabu sio civilized na hawana culture mbona wewe uliyekuwa civilized na ulikuwa na culture maarufu duniani hauna shirika lako la ndege?au una chuki zako za kibinafsi na hao waarabu?
    Fungua shirika lako la ndege lililokuwa Civilized halafu sie tutasafiri nalo.

    ReplyDelete
  21. Kuhusu kupotea mizigo hata mimi Kenya Airways wameshanipotezea mabegi yangu mara mbili, na juzi tu nilipokuwa transit Nairobi nikitokea Dubai begi langu nimelikuta limefunguliwa zipu kiujanja na kuibiwa vitu ndani,matatizo haya ni Airline zote sio Qatar au KLM yote ni sawa tu. kwenye kusafiri kwangu nimeshawahi kutana na watu wengi tofauti wa mataifa mbalimbali wao pia wanalalamikia upotevu wa mizigo na pia huduma mbovu.

    ReplyDelete
  22. Huyo mdau wa hapo juu,anayesema kwamba waArabu si wastaarabu,inaonekana ana chuki binafsi na race hiyo! Aache tabia ya ku-generalise mambo. Kwaiyo akisababishiwa usumbufu na mTanzania mmoja,atasema waTanzania wote si wastaarabu?!

    Acha ujinga wewe,tumia kichwa chako vizuri na acha kabisa kutema pumba!

    ReplyDelete
  23. Mliotendewa mazuri na QATAR msikatae maoni ya waliotendewa ubaya. Kwa ujumla QATAR sio ndege ya kupanda. Baadhi ya wadau wamesema ni wabaguzi wa rangi. Hiyo ni kweli kwani yalinikuta siku nilipokuwa narudi nyumbani. Sikukata tamaa nilisafiri nao tena wakati narudi ughaibuni na safari hii ubaguzi ulikuwa umepungua kidogo. Wadau wengine wamesema hao jamaa wanabambika watu makosa ambayo yanatokana na kuficha baadhi ya taarifa kwenye kukata tiketi, hili nalo lilinikumba. Hayo pia yalinikuta siku si nyingi pale airport ya Dar. Walitaka kufuta safari yangu nikakomaa sana mpaka mwisho ndege inataka kuondoka wananiambia nitoe kitu kidogo. Pamoja na kwamba kitu kidogo walichoomba kilikuwa kwenye uwezo wangu lakini nilichukia kwa nini wanifanyie huo mchezo? Nilighadhabika sana japo mwisho niliweza kusafiri. Kilichoniudhi zaidi ni pale ambapo taarifa walizotaka zilipaswa kutolewa wakati wa kukata tiketi na hawakufanya hivyo kwa makusudi kabisa. Kuna mdada mmoja mtu wa kaskazini kwa wala ndizi ndiye aliyekuwa kwenye usukani wa hilo sakata na hata walipomuita yule muhindi wa Qatar naye akawa upande wa huyo dada. Sina hamu nao niliamua kuachana nao nijaribu ndege nyingine nione kama wote wako hivyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...