Washiriki wa mashindano ya Mercedes Cup 2012 ya Boti zinazokwenda na Upepo (Sailing Boat) wakiwa wamekusanyika Yatch Club jijini Dar kabla ya kuanza mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors yanayofanyika kila mwaka.
Pichani ni Boti zinazotumika katika mashindano hayo.
Washiriki wakianza mashindano hayo kuzunguka fukwe karibu na kisiwa cha Bongoyo. Picha zaidi BOFYA HAPA


Yale yaleeee...wazungu ndo washiriki...wabongo tunazidi kutengwa na vitu kama hivi...haitachukua muda wenzetu hawa wajanja tutakuwa kama South Africa...umasikini utatukumbaaa mpaka basi...!! Mdau, USA-CA
ReplyDeleteAcha hizo wewe mdau hapo juu,ungekuwa member na wewe ungeyajua hayo.Yatch club ni kwa members tuu,wazungu wakitoka maofisini wanaenda sehemu za starehe na michezo walizojisajili na ni kwa kila mwaka unatakiwa kurenew uanachama wako.wabongo mkitoka ofisini mnakimbilia bar,lazima mpitwe.tuu!!!
ReplyDeleteWewe nenda uombe udhamini wa Vodacom kama huyo mzungu/muindi alivyopata kama hata watakusikiliza.
ReplyDeleteWazungu ndio kawaida yao, hutafuta mambo ambayo yatawatenga na walala hoi maana kama huna pesa huwezi kushiriki huo mchezo. Wako TZ lakini wanaishi kama UK.
ReplyDelete
ReplyDeleteSiyo kwa wazungu tu!
Baba yangu was a member yatch club DSM during early 70s na he had his own boat he made himself. We used to go there. Na ni wazaramo.
Kwa anaetaka kuna conditions if you meet unakaribishwa.
Sisi ambao "siyo wazungu" tuna interest zetu, na hao wazungu wako na interest zao.
Sisi tukitoka kazini ni Bar kwa kiti moto mbele kwa mbele halafu vikijitokeza vitu kama hivi tunaona tunatengwa wakati hatuna interest.
Manka Moshi kasema kweli kabisa.
Ujanja kukaa mabaa mpaka usiku wa manane.
Ukweli kabisa, toka 1970 wali kuwa wanachama waTanzania wana biashara.Mimi binafasi nili kuwa nina fahamu waTanzania walio kuwa wanachama.Mara nyingi nilikuwa nina alikuwa. Tusi walaumu wazungu,siku hizi ni mambo ya ujinga na ujanja. Wana biashara wazamani walikuwa tafauti.
ReplyDeleteMADIASPORA:
ReplyDeleteWandugu mliopo Majuu kama mnavyoona Bongo Tambarale na mambo yote mliyonayo na zaidi tunayo hapa hapa chini ya Mifenesi Bongo!
Mambo haya ni ya Daytona Beach-Florida, Miami Key west, San Diego beach California, Camp Davis Rhode Island, Cane-France, Napoli-Italy, Sicily,Palermo-Italy na Bilbao-Spain.
Yatch ndio kama hizo hapo, sea cruising rudini nyumbani mje mustarehe!, kama ni mahitaji mengine zaidi ya hilo hata kwetu wapo!
Kwani wazungu hawakai baa, hawa jamaa wabaguzi tu
ReplyDeleteSi lazima uingie Msikitini au Kanisani au ktk Chaka la Tambiko kwa vile unaona waumini wanaingia.
ReplyDeleteStarehe gharama ndiyo maana wabunge wanangangania 'mashangingi' wewe unatembelea suzuki jimmy au unapanda daladala lakini hulalamiki.
Bahati mbaya ulimwengu ndo ulivyo huwezi kuwa na starehe ya viwango vya juu bila noti.
Waache wenye nazo watanue mie ngoja nielekee kilabuni nikapate kidumu cha mbege.
Mdau
Mashati , Rombo
Mdau hapo juu mwenye malalamiko ya kutengwa.
ReplyDeleteTunafahamu kina Mzee Mwakitwange Mzaramo na wengine enzi za utawala wa Mwl. Nyerere walikuwa na yatch zao na pia wanachama wa Yatch Club.
Hivyo kama unazo na wewe nenda ukanunue ka-yatch au ufuate masharti ya uanachama wa klabu hiyo ili wewe pia ufaidi.
maana inaonekana unazo pesa ila hujiamini kujiunga na klabu hiyo hata kwa kukodisha unaweza kuendesha hicho chombo cha yatch.
Inaonekana umgeni jijini, uliza wenye mji utapatiwa historia A to Z ya jiji hili la Dar.
Kweli kuna haja kuanzisha vipindi maalum vya redio/tv ili watu wapate ufahamu wa historia ya miji mbalimbali ikiwemo Dar ilikuwa vipi 1930,1940, 1950, 1960,1970, 1980.
ReplyDeleteHistoria ya Yatch klabu kama wadau wengi walivyojaribu kuwaelewesha walioingia mjini miaka 1990 wakati mji ni mpana sana hivyo vitu vinavofanyika vitongoji vingine hawavifahamu. Naanza na yatch club kuongezea yale ambayo yameshabinishwa wa watoto wa mjini'
The Dar es Salaam Yacht Club was founded in 1933 on the waters’ edge of Dar es Salaam harbour by some keen sailing members of the then Dar es Salaam Club (the location is now the Forodhani Hotel on Kivukoni Front).
The club remained in the harbour until 1967 when it moved to the present site of Leopard’s Cove in the clean waters of Msasani Bay.
From a purely sailing club it set up the power boat section and then the diving section, which was originally a branch of the British Sub Aqua Club.
Mtoto-wa-Mujini
Leopold Cove huko 'Masaki' ilijulikana kama 'Kichanga Chui'.
ReplyDeleteMiaka hiyo ilikuwapo Oysterbay na Kichanga- Chui (ambayo sasa mnaiita Masaki).
Majina ya vitongoji kama kwa Pipino na kadhalika ya jijini Dar si wengi wanayafahamu maana sisi tumekaa kimya.
Tutaendelea kuibua historia ya jiji 'letu' kama ilivyokuwa kabla ya mji kuanza kupanuka na 'kujaa' miaka ya 1980.
Mdau
Sehemu za kwa Pipino
Dar-es-Salaam