Mwandishi wa Habari Mwandamizi Jenerali Ulimwengu akizungumza na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba (hawapo pichani) wakati alipokutana nao leo. Agosti.2012 na kubadilishana nao mawazo na uzoefu. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba, Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Katibu wa Tume hiyo Assaa Rashid.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadilko ya Katiba Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba (kulia) akizungumza na wajumbe wa Tume hiyo katika ofisi za Tume jiji Dar es Salaam wakati walipokuwa wakibadilishana mawazo na Mtaalamu wa historia na Mwanaharakati wa siku nyingi kutoka Zanzibar Profesa Abdull Sheriff (katikati) leo. Kushoto ni Mjumbe wa Tume hiyo, Dkt. Salim Ahmed Salim.
Mtaalamu wa historia na mwanaharakati wa siku nyingi kutoka Zanzibar, Profesa Abdul Sheriff (kushoto) akifafanua jambo katika mkutano wa na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu Joseph Warioba, Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Katibu wa Tume hiyo, Assaa Rashid (kulia).
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Humphery Polepole akiongea katika mkutano kati ya Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Mwanasheria na Mwandishi wa Habari wa siku nyingi Bw. Jenerali Ulimwengu. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Suleiman Omary Ali akiongea katika mkutano kati ya Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Mwanasheria na Mwandishi wa Habari wa siku nyingi Bw. Jenerali Ulimwengu. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Tume ya Katiba)
Na Mwandishi Wetu
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wameendelea kukutana na kubadilishana mawazo na uzoefu na Wataalam mbalimbali kuhusu Katiba Mpya kwa lengo la kuongeza uelewa wao na leo, kwa nyakati tofauti, Wajumbe wamekutana na Prof. Abdul Sheriff na Ndg. Jenerali Ulimwengu.
Tayari Tume hiyo imeshawaalika na kukutana na kwa nyakati tofauti na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa kwanza mzalendo Jaji Mark Bomani, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Pius Msekwa na Mhadhiri wa Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Issa Shivji.
Prof. Sheriff ni mtaalam wa historia na mwanaharakati wa siku nyingi kutoka Zanzibar na kwa muda mrefu amekuwa akishiriki na kutoa mada katika makongamano mbalimbali yanayohusu Katiba. Ndg.Ulimwengu ni Mwanasheria na Mwandishi wa Habari wa siku nyingi ambaye pia ameshiriki na kutoa mada katika makongamano mbalimbali yanayohusu Katiba Mpya.
Akizungumza wakati akiwakaribisha, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatambua kuwa Tanzania ina wataalam wanaoweza kutoa mchango mkubwa katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba na kuwasihi wanapopata nafasi wasisite kuwasilisha maoni yao kwa Tume.
“Tukipata nafasi, huwa tunawaomba wataalam kama ninyi kuja kubadilishana mawazo na Wajumbe wa Tume. Ni matumaini yangu kuwa Wajumbe wa Tume watafaidika sana na utaalam wako katika kupanua mawazo,” alisema Jaji Warioba katika mkutano uliohudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Agustino Ramadhani, Wajumbe wengine wa Tume na Sekretarieti ya Tume.
Jaji Warioba aliongeza kuwa Tume imejiwekea utaratibu wa kukutana na makundi mengine mbalimbali ya kijamii kwa lengo la kubadilishana mawazo na kupokea maoni yao kuhusu Katiba Mpya.
Akiongea katika mkutano huo leo (Jumatatu, Agosti 13, 2012), Prof. Sheriff pamoja na kushukuru kwa kualikwa na Tyume, alizungumzia uzoefu wake katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba unaoendelea na kutoa maoni yake katika masuala mbalimbali yakiwemo Muungano na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Kwa upande wake, Ndg. Ulimwengu ambaye amekutana na Tume hiyo leo mchana, pamoja na mambo mengine, alizungumzia umuhimu wa kuandika Katiba Mpya itakayotumiwa na Watanzania kwa miaka mingi ijayo katika kuwaletea maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Mbona kamati hii inakutana kila mara na watu wale wale kama kina Dr. Salim. Kamati hii inatakiwa ikutane na watanzania wa Marekani, Uingereza, Uchina na Australia. Hata wao wana haki ya kikatiba ya kutoa maoni.
ReplyDeleteKweli kabisa...hiyo kamati ije huku ugaibuni ipate mawazo chanya..hao wenyewe walikaa kimiya wakati watz wakiumizwa...na kipengele kiwekwe hata wadosi na warabu watoto wao iwe kitu cha kawaida kuolewa na watz na kuzaa nao..mashule yao watoto wetu wasome pasipo na masharti yoyote..watoke upanga wakaishi hata tandika..manzese..na vijijini pia wakashike jembe kama watz..sio walimiwe tu nakula...matajiri wabanwe kusiwe na tabaka la tajiri na masikini..mnao simamia maoni ya katiba myaone hayo msimuonee mtu aibu ili muokoe kizazi chetu cha kitz..ni hayo tu kwaleo...ni mm tajiri wa mawazo endelevu...sikusoma ila naona mbali...amani kwa wadau wote.
ReplyDeleteduh huyu naye kadandia treni.sasa dr salim si ndo kamati yenyewe.duh kazi kweli kweli
ReplyDeleteMTOA MAONI No3 INAONESHA WAZI ULIVYOMBAGUZI, MCHOYO NA ROHO MBAYA. ETI WAHINDI NA WARABU, KWANI HII NCHI UMEAMBIWA YA WATU WA AINA GANI? MBUZI ANAKULA KUTOKANA NA UWEZO WA KAMBA YAKE SIO KILA MTU UMLAZIMISHE LAZIMA AFANYE HIVI, TUNATAKA NCHI IWE YA DEMOCRACY HATUTAKI UBAGUZI WA AINA YOYOTE. MTU AWE HURU KATIKA NCHI YAKE LAKINI AFATE SHERIA ZA NCHIKAMA MTANZANIA.
ReplyDeleteDkt. Salim Ahmed Salim ni mmoja kati ya Wajumbe 32 wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Wadau waliopo ughaibuni wanaweza kuwasilisha maoni yao kupitia tovuti ya Tume (www.katiba.go.tz) au facebook 'Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania' au S.L.P. 1681, Dar es Salaam au S.L.P. 2775, Zanzibar
ReplyDeletesisi tunataka wakutane na Tundu Lissu na Dr.Slaa. kwanini tume inawaita makada wa CCM tu kama Ulimwengu,na Mark Bomani??
ReplyDeleteAnyn namba 2; hayo ndo mawazo chanya kweli??! To me, these are the worst opinions i've ever heard in my entire whole life! Halafu unajitapa eti upo ughaibuni na mawazo yako chanya!
ReplyDeleteKama ulishindwa kuoa mtoto wa kiarabu na wa kihindi, hilo ni tatizo lako binafsi. Mbona wengine wanaoa?!Hebu tudokeze, huko ughaibuni unakobeba boksi, katiba za nchi zao zina address hayo uliyoyainisha hapo juu??!