TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange kuomboleza vifo vya askari wawili wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) waliokuwa wanalinda amani katika eneo la Darfur, Sudan, vilivyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita.
Katika salamu zake hizo, Mheshimiwa Rais Kikwete amemwambia Jenerali Mwamunyange: “Nimepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za vifo vya vijana wetu watatu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) ambao walikuwa wanalinda amani katika Darfur, Sudan ambavyo nimejulishwa kuwa vilitokea Jumapili iliyopita.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Vifo vya vijana wetu hawa vinasikitisha zaidi kwa kuzingatia kuwa wamepoteza maisha yao katika utumishi muhimu sana wa nchi yetu na katika kulinda amani ya Bara letu la Afrika. Tutaendelea kuwakumbuka kwa utumishi uliotukuka na mchango wao kwa nchi yetu na kwa Bara letu la Afrika.”
Amesema Mheshimiwa Rais Kikwete: “Kufuatia vifo hivyo, nakutumia wewe, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange salamu za rambirambi. Aidha, kupitia kwako, naomba uniwasilishie pole zangu nyingi kwa familia za vijana wetu ukiwajulisha kuwa moyo wangu uko nao wakati wa kipindi hiki kigumu cha kuwapoteza wapendwa wao. Naungana nao kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aziweke pema peponi roho za marehemu.”
Rais Kikwete pia amemtaka Jenerali Mwamunyange kuwafikishia salamu za pole Makamanda na askari wote wa Tanzania wanaolinda amani katika Darfur.
Askari hao wawili ambao ni sehemu ya wanajeshi 850 wa Tanzania wanaolinda amani katika Darfur na mwenzao mmoja ambaye hajulikani alipo mpaka sasa walipoteza maisha yao katika ajali ya gari lao kusombwa na maji wakati wakivuka mto katika Kijiji cha Hamada, eneo la Manawasha, Darfur.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
28 Agosti, 2012



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Paragraph ya kwanza inasema wawili, paragraph ya pili inasema wanajeshi watatu??? Je ndio zimamoto hata kwenye jambo rahisi kiasi hiki??

    ReplyDelete
  2. Anony Tue Aug 28, 08:42:00 PM 2012, soma habari kwa ufasaha.
    mwanajeshi wa tatu hajulikani alipo ila miili ya wawili i,epatikana.

    ReplyDelete
  3. Kama hajulikani alipo nani kampa taarifa rais kuwa huyo wa tatu naye amekufa?
    Bado nikosa kubali na urekebishe.Taarifa inapotosha,bora iwe 2wamekufa na 1 hajulikani alipo.

    ReplyDelete
  4. Jamani kama ni Gari lao kusobwa na Maji, Twahitaji kujumuisha mafunzo ya kuogelea katika " package" ya mafunzo ya kijeshi, Labda kama mniambie waliingia kwenye mtego wa adui hapo sawa, lakini kama ni maji tu,Napenda kuchukua nafasi hii kumwagiza mkuu wa mafunzo ya Jeshi JKT na TPDF arekebishe Silabasi yake na kujumuisha mafunzo ya kuogelea katika Silabasi hiyo.
    Mwisho natoa pole kwa Watanzania na familia za marehemu. Bwana awape marehemu raha ya milele na mwanga wa milele uwaangazie,wastarehe kwa amani, Amina.

    ReplyDelete
  5. Nini vita ya Darfur huko?

    Hakuna sababu ya kupoteza Askari wetu muhimu kwa vita za nchi zingine kwa nini tusitume Majeshi kuipiga Malawi kwa kudai sehemu yetu ktk ziwa Nyasa?

    ReplyDelete
  6. Yaani bado serekali inatumia yahoo kama email ya mawasiliano?? Ndio maana info za muhimu zina-leak kirahisi. Kweli bado sana ....

    ReplyDelete
  7. Wanajeshi walikwenda Komoro kwa kulinda amani pia mmoja akafa maji, tatizo nini?

    sesophy

    ReplyDelete
  8. wabongo hauna jema!!kulalamika tuuuu ndio maana masikini!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...