Na Geofrey Tengeneza –Yeosu Korea
Siku yaTaifa la Tanzania katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Korea yanayofanyia katika jiji la Yeosu hapa Korea iliyofanyika tarehe 8/8/2012 iliweka historia na kuvutia maelfu ya wananchi wa Korea na watu mbalimbali kutoka mataifa mengine wanaoshiriki katika maonesho haya ikilinganishwa na siku mataifa mengi hususan kutoka barani Afrika.
Siku ya Tanzania ilianza kwa maandamano ya watanzania wanoshiriki maonesho hayo sambamba na wale wanoishi hapa mjini Yeosu yakiongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Dkt. Abdallah Kigoda yakianzia katika eneo maalumu la VIP ililo karibu na geti kuu la kuingilia katika viwanja vya maonesho hayo majira ya saa nne asubuhi yakipambwa kwa bendera ndogo zilizokuwa zikipungwa hewani na watanzania hao wakiongozwa ngoma ya Ngongoti iliyokuwa ikichezwa na kikundi cha ngoma kutoka Chuo cha Taifa cha Bagamoyo (TASUBA) huku maandamo hayo yakishangiliwa na maelfu ya wananchi wa Korea.
Hali ilikuwa ni tete zaidi katika ukumbi wa mikutano wa Maonesho hayo (Expo hall) ambapo maelfu ya wananchi wa Korea walianza kujikusanya mapema kabisa kuanzia saa 3.00 asubuhi kwa lengo ;la kuingia katika ukumbi ambao maandamano yangefikia huku wakigombea maelfu ya bendera ndogo , DVDs na vipeperushi mbalimbali vinavyoelezea utalii wa Tanzania vilivyokuwa vikitolewa na maafisa wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) , Shirika la Hifadhi za Taifa la Tanzania (TANAPA) na mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA).
Ni Korea ipi DPRK (Korea ya Kaskazini) au South Korea (Republic of Korea)?
ReplyDeleteMdau
Rufiji
na sisi wengine tunahitaji huku waje kuhamasisha watalii wa huku europe wanapenda sana hebu jaribuni tu kidogo muone mafanikio.
ReplyDeleteJamani kumbe kuitangaza nchi ni rahisi sana kimataifa basi uwekwe mkakati kabambe..nahao ttb.tanapa.ncaa..kwa nchi zote za ugaibuni..hayo ndio mambo yanayo takiwa.. ni mm tajiri wa mawazo endelevu uk...amani kwa wadau wote.
ReplyDelete