Mchezaji wa timu ya Simba akimiliki mpira mbele ya mabeki wa timu ya Nairobi City Stars ya nchini Kenya katika mchezo wa kirafiki wa kuadhimisha Tamasha la siku ya Simba (Simba Day) lililofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo liliandaliwa na klabu ya Simba na huwa linafanyika kila mwaka Agosti 8 kama ya leo na kushirikisha timu marafiki wa klabu hiyo huku wachezaji na viongozi mbalimbali wakipewa zawadi kwa mchango wao kwa klabu hiyo, Katika mchezo wa leo timu ya Simba imefungwa magoli 3-1.
Mchezaji wa mpya wa Timu ya Simba,Mrisho Ngassa akijiandaa kupiga mpira mbele ya Mabeki wa timu ya Nairobi City Stars katika mchezo uliochezwa leo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Simba (Simba Day) ambayo huwa yanafanyika kila Mwaka siku kama ya leo.Simba imefungwa Bao 3-1.
Danny Mrwanda wa Simba akijiandaa kumtoka beki wa timu ya Nairobi City Satrs.
Wachezaji wa Simba wakiwa hawaamini kitu kilichotokea uwanjani hapo.
Wachezaji wa Nairobi City Stars wakishangilia ushindi wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. uchawi na ujuzi (talent) haviingiliani. Simba jipangeni upya, mmemleta Ngassa kuongeza wachezaji wachawi klabuni kwenu, mtajiju na bado.

    ReplyDelete
  2. Hivi ni heri kuwa na viti vitupu tele kiasi hiki kuliko kuteremsha bei za kiingilio na watu kujaa uwanjani? Haingii akilini kabisa, bei za viingilio katika mechi kama hizi ni ghali sana kwa mtanzania.

    ReplyDelete
  3. simba hoi

    ReplyDelete
  4. Poleni watani! lazima tukubali kwamba Simba mwaka huu hamna timu nzuri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...