Katika Gazeti la Business Times toleo nambari 1248 la Ijumaa, tarehe 10 Agosti 2012, ziliandikwa habari zenye kichwa cha habari chenye maana kuwa “Operesheni za NBC zawekwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu”. Katika habari hiyo ilielezwa kuwa Benki Kuu imechukua hatua hiyo kufuatia ripoti za tuhuma kadhaa zihusuzo udhaifu katika uendeshaji wa benki na utawala bora.

Benki Kuu inapenda kuchukua fursa hii kuueleza umma kuwa haijaweka operesheni/shughuli za NBC chini yake. Benki hiyo inajiendesha yenyewe kwa kufuata utaratibu wa Sheria za Makampuni, 2002, Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha 2006 na miongozo itolewayo na Benki Kuu kama zilivyo benki zingine. Wateja wa NBC na Umma kwa ujumla wanashauriwa kuendelea kufanya biashara na benki hii kama kawaida.

IMETOLEWA NA BENKI KUU YA TANZANIA
11AUGUST 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mie niliisoma hiyo habari na jinsi ilivyokua makini na ukizingatia na aina ya gazeti sikua na shaka yoyote,nilijua ni kweli. Kumbe hata the so called "serious newspapers" sasa wanaandika udaku? Ni huo ushindani au nini? Tuende wapi sasa kwa habari za kuaminika? The fourth estate needs a thorough house cleaning!

    ReplyDelete
  2. Some news papers in this country are so irresponsible and have no regard whatsoever to the welbeing of our economy. Publishing such unfounded story could easily cause bank run and ruin our economy!

    ReplyDelete
  3. Hii taarifa haijitoshelezi. Haijafafanua zaidi tunaomba details tafadhali.

    ReplyDelete
  4. Hapa napata picha Kuwa asilimia kubwa ya magazeti ya Tanzania hayaripoti ukweli nanhayafuati maadili ya uandishi Wa Habari. Katika gazeti la Mwananchi la Jana tarehe 11 august 2012 kuna tangazo lilitolewa na wizara ya Maui likikanusha Habari zilizoandikwa na gazeti la Rai na Mwananchi pia. Wiki hii pia Itv Waliomba radii kutokana na Habari waliyoitoa ambayo ilikiuka haki Za mtoto. Jamani tunaelekea wapi? Wizara ya Habari iko wapi na inafanya nini? Naishauri serikali isilifumbie macho jambo hili kwani likiachwa Kama lilivyo litaipeleka Nchi pabaya kwani vyombo Vya Habari vinanguvu sana ya kushawishi jamii. Maoni yangu Mimi Ni hayo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...