George madaha malongo
1940-11-06 - 2009-08 -07
Ni miaka mitatu (3) sasa tangu ulipotuacha kwa machungu mengi. Daima tunamshukuru mungu kwa muda wote uliokuwa nasi; Sio tu kuwa Baba mwenye upendo bali kwa kuwa ulikuwa mtuwa pekee miongoni mwetu. Uliyobarikiwa kwa mambo mengi, ucheshi wako, hekima yako, na juu ya yote hayo ulikuwa unafanya jambo kwa kusudi maalumu, na kuwataka watoto wako wote wawe/ tuwe na upendo.
Tutaendelea kukumbuka na kufuata ushauri wako na mema mengi uliyotufundisha, na tutaendelea ukumbuka busara zako.
Daima unakumbukwa sana na mke wako mama Rhoda malongo; watoto wako wote; wajukuu zako wote, vitukuu vyako; wadogo zako wote; marafiki wako wote; majirani zako wote. Familia yote ya malongo tunapenda kutoa shukrani zetu wote kwa ndugu na marafiki wote kwa upendo walionyesha wakati wa kipindi kigumu tulicho kuwa nacho.
Bwana alitoa Bwana alitwaa, jina la bwana lihimidiwe milele AMEN.PUMZIKA KWA AMANI-AMEN.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...