Washambuliaji wa timu ya taifa, (Taifa Stars) Mrisho Ngassa (kulia) na Haruna Moshi Boban wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ajili ya safari ya kwenda Gaborone, Botswana kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kesho Jumatano.
Nohodha wa timu ya Taifa,Taifa Stars Juma Kasseja akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa kupanda ndege kwenda Gaborone, Botswana kwa ajili ya mechi ya kimataifa ya kirafiki itakayochezwa kesho Jumatano.
Wachezaji wa timu ya Taifa, Taifa Stars wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa kupanda ndege kwenda Gaborone, Botswana kwa ajili ya mechi ya kimataifa ya kirafiki itakayochezwa kesho Jumatano.





Kila la heri Stars.Chezeni kwa bidi ili kushinda,mkishinda ugenini ni rahisi kupata mialiko kutoka kwenye timu nyingine Vigogo duniani.
ReplyDeleteDavid V
wanaenda kufanya nini huko..poteza muda tu na mafuta ya ndege na pesa..
ReplyDeleteKila la kheri taifa stars ,wachezaji jitumeni na kuipeperusha vema bendera ya taifa.Mdau hapo juu unaonekana hauna uzalendo na sio mwanamichezo ,je fani yako nini?Big up mdau ,big Joe
ReplyDeleteMsizamie tu huko mtachinjwa
ReplyDeleteHajabu, yaani Ngassa, Nyosso, Kaseja, ni wachezaji wa taifa kweli? Najiuliza kwa mpira upi? Sasa hapa tunategemea nini ikiwa wachezaji wenyewe ndo hawa? Kumbukeni, uchawi na vipaji ni vitu viwili tofauti kabisa.
ReplyDelete