Nyota wa Kikapu, Tyson Chandler Mchezaji mahiri wa kikapu toka Marekani anayechezea timu ya New York Knicks kama "center" na pia anachezea timu ya Taifa ya Marekani yuko jijini Dar Es Salaam kwa ziara maalumu.

Tyson yumo kwenye timu ya Taifa ya Marekani iliyotwaa medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki ya 2012 yaliyomalizika London na alicheza michezo yote.

Tyson ambaye msimu huu wa ligi ya NBA iliyoisha alichaguliwa kuwa mchazaji bora  mzuaji/Mlinzi (NBA Defensive Player of the year) pia ni balozi wa heshima wa UNICEF.

Katika ziara ya Dar amefanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kutoa mafunzo ya kikapu kwa vijana wadogo/ watoto wa mitaani katika viwanja vya Don Bosco.

Tunamshukuru sana Tyson na pia tunawashukuru UNICEF kwa ushirikiano wao. Pichani anaonekana Tyson akiwa Don Bosco wakati wa mafunzo kwa vijana wadogo/watoto wa mitaani na picha nyingine ni Mkurugenzi wa Michezo na Ushirikiano wa UNICEF USA akiwa na Magesa/TBF-VP.

Phares Magesa
Makamu wa Rais,
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania(TBF).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. kwa kweli baskteball tunapoteza muda wetu tu. maumbo yetu ni madogo sana kucheza mchezo huo.tuweke nguvu kwenye riadha. tena mbio za kati na ndefu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...