Ndugu Issa Michuzi na wadau wengine wote wa blog ya jamii.
Binafsi nimeguswa sana, tena sana, na wimbi la ajali ambalo limegeuka kuwa kama sehemu ya kawaida tu ya maisha yetu Watanzania. Naumia sana ninapoangalia zaidi ya picha za ajali, pale ninapoona familia za wahanga zinapofikishiwa taarifa kuwa "mzazi wako amefariki" au "mwanao hatunaye tena" au "mkeo/mumeo katutoka" n.k. Zaidi pia na mabadiliko ya ghafla katika maisha, tena mabadiliko yasiyotarajiwa na yenye kutia uchungu sana, kwa waliofiwa. Kuna ambao wanaathirika sana kisaikolojia, kiuchumi, kiafya na kijamii kwa ujumla. Inauma sana, kisa tu basi fulani ama lori fulani lilitaka kuwahi mbele ya jingine ama kukamilisha safari mapema zaidi, au tu kujionesha kuwa lenyewe ni bora zaidi ya mengine. Ninapozungumzia basi ama lori ninamaanisha madereva husika.
Wadau wengi wamependekeza hatua kadhaa zinazoweza kupunguza ajali nchini, zikiwemo za muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu. Ninawaunga mkono kwa dhati kabisa, kwani nia yao ni njema sana. Nami nimeona niongeze namna moja ambayo inaweza kusaidia katika fikra za viongozi wetu kutatua ama kupunguza ukubwa wa tatizo hili.
Napendekeza kuanzishwa kwa taasisi ama idara maalum katika taasisi iliyopo tayari (hasa SUMATRA) ambayo itaendesha mabasi na malori kutokea ofisini kwa kutumia kompyuta. Mabasi na malori yabandikwe kifaa maalum ambacho polisi wa usalama barabarani, abiria na raia kwa ujumla wataweza kukiona, kifaa ambacho kitatoa taarifa za basi ama lori. Taarifa hizo zimtambulishe dereva, mahali ambapo basi ama lori lipo likiwa katika mwendo, mwendo kasi wa basi ama lori, na kama linaovateki ama la na hali ya barabara ilivyo kuruhusu hilo. Hawa jamaa waliopo ofisini waweze kumuonya dereva asivunje sheria kwa kutuma ujumbe kupitia kifaa kilichobandikwa kwenye chombo cha usafiri (kipige kelele sana na kila mtu asikie). Akiendelea na kuvunja sheria, hata kama hakusababisha ajali, achukuliwe hatua ikiwemo na kunyang'anywa leseni na kushitakiwa. Mmiliki wa basi pia aadhibiwe kwani anapaswa kuwa mkali kutowaruhusu madereva wake waendeshe kimauaji. Polisi wa usalama barabarani wahakikishe basi ama lori lina kifaa hicho na kinafanya kazi wakati wote.
Hatua hii inaweza kuanzia na mabasi na malori yanayotia mguu kwenye barabara kadhaa tu kwanza (hasa barabara zinazohusika sana na ajali). Uwekezaji katika teknolojia ya namna hii unaweza kuwa wa gharama lakini una thamani kubwa kuliko pesa. Tuwasaidie watoto wasipoteze wazazi wao, wazazi wasipoteze watoto wao, n.k.
Kumradhi endapo wazo hili litawakinai baadhi yenu. Mimi si mtaalam wa masuala haya bali najaribu tu kuchangia kile ninachoona kinaweza kutusaidia sote.
Asanteni
Mdau, Canada.

uzuri wa hoja yako ni kuwa unajaribu kutafuta solution ya tatizo sugu linalotuumiza sote.Napenda awali kukupongeza kwa rai yako japo sina utaalamu wa jinsi gani hoja yako inavyoweza kutekelezeka.Nadhani kwa kufuata msingi mzuri uliouweka wapatikane na wengine wenye hoja za kiutautuzi kisha wahusika na wataalam wakae waangalie ipi ni hoja sahihi itayotusaidia zaidi katika kujiokoa na balaa hili linalotukumba kila siku kizembe sana
ReplyDeleteMdau,
ReplyDeleteUtatuzi wa hii problem ni very simple.
Wafunge "SATELLITE CAR/ TRUCK TRACKING DEVICES" kwa mabasi yote.
Karibu wamiliki wa malori ya mafuta yote wanafanya hivyo.
Wanaweza kuona mwendo/speed ya gari wakiwa maofisini mwao through the computer. Na wanachukuwa hatua zipasazo panapo tokea makosa.
Ajali zinazohusu malori ya mafuta zimepungua kabisa. Chache zilizopo ni zile unavoidable.
SUMATRA au traffic police wanaweza kabisa kutekeleza uwekaji wa vyombo hivyo kisheria. Wakawa wana monitor wakiwa maofisini kwao!!!
Tatizo...... hapo itawaondolea ulaji ma traffic barabarani!
Satellite car tracking devices ndio suluhisho.
ReplyDeleteSumatra na traffic police itawapunguzia kazi kwa ku- monitor hawa wenda wazimu wanaotumalizia familia zetu kila kukicha!
Sio ghali hivyo. Na uzuiaji wa ajali na mauwaji ya kizembe inapita na kuzidi gharama zozote za kifedha.
Jamani tumechoka kwenda matangani kila siku!
Hebu wahusika angalieni hilo....
Mdau kuna mkakati wa kufunga kifaa kiitwacho CAR TRACKING SYSTEM na taarifa nilizonazo ni wamiliki wa mabasi nchini wanakipinga kwa nguvu zote!!
ReplyDeleteMpinga na Mzee Kilima tafadhali harakisheni ili mtuokoe na ajali hizi waheshimiwa, misiwasikilize wamiliki hawa ambao wanadanganywa na madereva wao.
Nakubaliana na wewe na pia maoni ya wote katika blog hii lakini kitu kikubwa cha kufikiri ni jinsi ya kubadili utamadunu wa kibongo kwa kuchukulia mambo 'serious' Nakumbuka mabasi yalifungwa speed governor miaka ya 90 lakini madereva na polisi walishirikiana kupuuza chombo hiki. Ninakumbuka polisi kusimamisha gari kwa sababu tulifika Mombo kabla ya saa na konda alitoka kwa dakika kumi tu akarudi anatabasamu na speed ni ile ile!
ReplyDeleteNi sheria kwanza kwamba ni jinsi gani mtu ataharibu kibarua chake popote akikiuka sheria. Lakini Tz hatuna uthibiti wowote! Kuanzia ufisadi. Wangapi wameitwa wafisaidi au wamekamatwa wafisadi na wakahamishiwa tu idara nyingine na mtindo ni ule ule!
Pole mdau unasound polite lakini Utamauni wa WaTz na kufuata sheria haujazaliwa bado. Hata zikiwekwa zitavunjwa tu hadi utamaduni huo utakapozaliwa.
Na mimi nakubaliana na maoni yako mdau wa Canada na maoni yote hapo juu.Kama alivyosema kiongozi mmoja hapo juu-UTAMADUNI WETU-Hatutaki kubadilikia....Na hapa ndipo tatizo lilipo.Tulivyo wa ajabu hizo system lazima zitakuwa interupted tu ama na watu wa IT au "kuzichezea" tu zisifanye kazi kwenye magari.Wakati wanaleta hizo system,ninavyowafahamu waTZ kuna kundi jingine hapo limeshajiandaa -'kuzifanyia kazi' ili zisifanye kazi,matajiri wa mabasi wanakuwa wanalilipa hilo kundi.SHERIA ZIWE KALI TU,SABABISHA AJALI kizembe kamata peleka jela miaka 15-30. kwisha.
ReplyDeleteModou
mimi nashauri vitu hivi vitano vitiliwe mkazo kwanza ndipo hiyo teknologia itafanyakazi vizuri.
ReplyDelete1.ELIMU KWA WOTE; wananchi wote wapewe elimu kuhusu matumizi bora ya barabara, sio kung'ang'ani madereva tu, hata watumiaji wengine pia waelimishwe hata maafisa wa usalama barabarani, mfano, katika barabara kuu ziendazo mikoani si jambo la ajabu kukuta watu wamekaa chini kwenye ukingo wa lami wanapiga soga, hawa wanaitaji elimu, au mtu anavuka barabara kwa kujivuta huku gari inakuja au afisa usalama barabarani anasimamisha gari akiwa amesimama katika ya barabara.
2.SHERIA YA OVERTAKE; sheria hii isimamiwe kwa nguvu zote hasa katika kipengele hiki, iwapo gari itakuwa inaipita nyingine,dereva wa ile inayopitwa ajitahidi kuipisha ile nyingine kwa kusogea kushoto zaidi kama inawezekana na apunguze mwendo kuiruhusu impite na sio kuongeza mwendo (wenyewe wanaita kumwashia) kuizuia isimpite, iwapo afisa wa usalama barabarani atashuhudia gari inayopitwa ikizuia nyingine kupita kihuni basi dereva wake aadhibiwe vikali.
3. PARKING. namna ya kuegesha magari, kila dereva ajitahidi kuegesha gari pembeni zaidi kadiri iwezekanavyo. iwapo itabainika kuwa dereva ameegesha barabarani kizembe basi aadhibiwe. kwa yale yaliyoharibika barabarani yapewe muda wa kutolewa barabarani kuwekwa pembeni kulingana na tatizo, muda ukipita yaanze kutozwa parking.Hili lifanyike kwa busara kwa faida ya pande zote mbili aliyeharibikiwa na watumiaji wengine.
4.Sheria zirekebishwe ili zimuadhibu mtenda kosa mwenyewe, ukisoma maoni mengi humu utaona wamiliki wanalaumiwa sana, lakini tujiulize dereva anapofanya kosa wami, mmiliki yupo moshi, anahusika vipi? dereva kaendesha kwa mwendo wa kasi kawahi kituoni, gari inapigwa faini analipa mmiliki, kosa kafanya dereva, huyu dereva atajirekebisha kweli?
5.UBORA WA BARABARA; barabara zitanuliwe, barabara zetu nyingi nyembamba, ili maroli mawili yapishane lazima upande mmoja yakanyage nje ya barabara, hii si salama, sehemu zote ambazo barabara ni pana, ajali ni chache sana, mfano kipande cha chalinze-morogoro, iyovi-kitonga, hata kilima cha ukonga magereza ajali zimepungua sana tangu barabara itanuliwe. pia zijengwe kwa ubora na kuzingatia usalama, mfano kipande cha barabara cha kisarawe mkoa wa pwani mpaka kiwanda cha saruji Mpuyani usalama huakuzingatiwa kwani mkandarasi aliyeweka lami naamini ni mtandika lami tu si mjenzi wa barabara kwasababu kuna kona nyingi tu ambazo alitakiwa azipunguze ukali lakini ameziacha.
mwisho naomba elimu kuhusu hili la mwendokasi, mnaposema mwendo kasi mna maana gani? kwa dereva mwanafunzi mwendo wa km 30/saa ni mwendokasi, kwa Schumacher dereva wa mbio za magari km 130/saa ni mwendo wa taratibu. sasa mwendo kasi ni nini?
mimi nafikiri kama watu wamwchoka ajali basi tuchukue jukumu wenyewe sisi abiria ambao ndio tunaokufa. Gari linapoendeshwa kwa kasi abiria wote wamchangamkie dereva wamwambie aendeshe kwa nidhamu au mnaamua kushuka au kupiga simu kwa mwajiri wake. Police mnapokutana nae njiani ni kuhakikisha hapewi hongo, nae nikumueleza kua hatutaki kuendelea na safari maana dereva wetu anaendesha bila kujali maisha yetu. Tukisubiri vyombo vingine viundwe na wenyewe waanza hongo kama mambo ya speed govener yalivyokua tutaendelea kupoteza maisha yetu na ya jamii inayotuzunguka. Abiria tuchunge maisha yetu kwa sababu serikali, waajiri na madereva wote wamelala. kazi kwetu jamani.
ReplyDeleteMadereva wa Tz hasa wa magari makubwa ni jeuri, wana nyodo, kaidi wanafikiriaga wao ndio wenye nguvu kumbe hilo jigari ndilo lenye nguvu, kama unabisha uliza trafiki wa nchi jirani. A moral decay we are in. afadhali kidogo Zenj kuna kujali sheria za barabarani. Tatizo ni u shosti na matrafiki.Hawakemei kwa shati. Ukicheke na kima utavuna mabua.
ReplyDeleteMdau wa Canada,
ReplyDeleteTuko pamoja na wazo lako ni zuri sana kwa kuwa hakuna kinachoshindikana chini ya jua isipokuwa umauti tu!
Changamoto zilizopo kwa suala hili:
1.Uwezo wa kitaalamu wa kupata huo mfumo utatusumbua.
2.Uwezo wa kifedha na urasimu pia ni tatizo nchini.
3.Aina ya Madereva tulionao wengi hawakusoma, zaidi ya hapo wana matatizo binafsi ya ki-hulka kama matumkizi ya ulevi hasa wakiwa kazini.
Hivyo vitatu hapo juu ndio vitakuwa changamoto kubwa sana kuifikia azma hiyo nzuri kabisa!
Wadau mmeongea vizuri. Kama wasimamiaji wa sheria wataacha nina uhakika ajali za kizembe kama zinazotokea zitakwisha. Pia mimi nina nyongeza moja kuwe na utaratibu kila dereva awe na pointi na dereva apunguziwe pointi kwa kila anapofanya kosa la barabarani. Akimaliza pointi zake atumikie adhabu ya mwaka mmoja halafu aende chuoni kusoma upya. Pia ili kuhakikisha hatua kali, kila polisi wanapomkamata dereva kafanya kosa au wananchi kuripoti uendeshaji mbaya wa dereva wa gari, leseni yake itobolewe na akifikisha matundu kadha arudi chuoni akasome upya. Na kipindi cha kusoma kwa madereva kama hao iwe mwaka mmoja. Ila muhimu wasimamiaji watende haki wasitengeneze mazingira ya rushwa. Watu tubadilike tusifurahie pesa zilizomwaga damu ya watu.
ReplyDeleteNaomba na mimi nichangie mawazo kidogo! juu ya Hili swala la ajali za barabarani haswa hizi njia kuu,zitokazo nje ya nchi,Dar-Arusha na Dar-Mbeya, linachangiwa sana na magari ya mizigo! Hivi sasa Tanzania tunategemea usafirishaji mizigo kwa njia ya barabara tu TAZARA imekufa! TRC imekufa!msongamano wa magari ya mizigo na abiria ni mkubwa mmno!na barabara zenyewe ni finyu mmno! hazina hata service road,gari moja likiharibika barabarani, basi hakuna njia ya pembeni ni msongamano tu!. mimi naona Tuelekeze nguvu zetu nyingi kufufua njia ya reli ili mizigo mingi isafirishwe kwa njia ya Reli.amasivyo kesho itakua zamu yako ama yangu kupata ajali!utasafiri tu!
ReplyDeleteMdau wa Canada unasema kweli, ni rahisi kifaa kinafungwa maana nasema hivyo hapa kazini kipo na magari ukizidisha mwendo tu kinapiga kelele inakuwa kero na kule monitor room wanatajua umezidisha ukirudi unaweza kunyangwanywa leseni. Na uzuri gari haliende bila kuweka card yako na kila ukiweka uko ofisini wanajua nani kawasha gari gani, likizidisha mwendo wako na wewe
ReplyDeleteserikali irudishe usafiri wa mkoa kwa mkoa chini ya KAMATA a.k.a Kampuni ya Mabasi ya Taifa ndiyo suluhisho na kupiga marufuku kampuni za usafiri za binafsi.
ReplyDeleteMaana nchi haiwezi kuwa na makampuni binafsi zaidi ya hamsini yanayoshindania faida kwa mwendo-kasi, mafundi na karakana hawana, dereva kuendesha zaidi ya kilometa 300 bila kupokezana n.k n.k
Kampuni ya Mabasi Ya Taifa itaka mzizi wote wa ajali-zembe, itawalipa mishahara mizuri madereva. Kila basi lenye safari zaidi ya kilometa 300 madereva wawili lazima na kama linakwenda zaidi ya kilomeya 700 madereva watatu kila basi pia hakuna umuhimu wa kondakta. Teknolojia pia muhimu kwa mabasi ya KAMATA.
Serikali haina uwezo wa kujenga barabara kama ya Nyerere Road (Pugu road) kuunganisha mikoa, hivyo mwendo taratibu wa KAMATA ndiyo dawa mujarabu kwa ajali hizi za mabasi ya kampuni binafsi.
Mdau
Gerezani ilipokuwa stendi ya Kamata