Mahmoud Ahmad Arusha

Serekali imetishia kuwatimua wawekezaji wa kampuni ya madini ya Tanzanite one iliyopo Mererani wilayani Simanjiro iwapo watashindwa kulipa deni la zaidi ya dola za kimarekani milioni 2.2 zilizotokana na ukwepaji kodi .

Katibu mkuu wizara ya nishati na madini Eliakim Maswi alitangaza msimamo wa serikali wa kupitia upya mikataba ya makampuni ya madini hapa nchini baada ya kugundulika kuwa yapo makampuni kadhaa yamekuwa yakiendesha shughuli zake za madini bila kulipa ushuru wa serikali kinyume cha sheria.

Akizungumza na chama cha wanunuzi na wauzaji wa madini nchini TAMIDA,jijini Arusha jana,Maswi alisema kuwa kampuni ya Tanzanite one imekuwa ikikwepa kulipa kodi ya mrabaha wa madini tangu mwaka 2004 hadi 2008 na kufikia kiasi cha shilingi bilioni 3.4 fedha za kitanzania.

Alisema kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikitumia ujanja wa kukwepa kulipa mrabaha wa mauzo pale inapokuta soko la madini nje ya nchi limeongezeka na kwamba serikali kupitia kitengo cha ukaguzi wa madini iliweza kubaini ukwepaji huo wa kodi na kuiamuru kampuni hiyo kulipa kiasi hicho cha fedha au ifungashe virago.

‘’tulibaini ukwepaji wa ulipaji kodi kwa kampuni ya Tanzanite one baada ya kuanzisha kitengo maalumu za ukaguzi wa migodi hapa nchini na tulipoifikia kampuni hiyo ndipo tulipobaini imekwepa kulipa kodi kiasi hicho,na hivi sasa tunaanza kupitia upya mikataba ya makampuni ya madini’’alisema Maswi

Aidha alifafanua kuwa kampuni hiyo iligoma kulipa deni hilo ikidai ni kubwa sana ,ndipo serikali ilipotaka kufanya ukaguzi upya ,kupitia wakaguzi wake , lakini kampuni hiyo iligoma na kudai kuwa ipo tayari kulipa deni hilo .

Aliongeza kuwa iwapo kampuni hiyo ingegoma kulipa deni hilo serikali ilikuwa tayari kuwatimua na kuwamilikisha wazawa mgodi huo.

Kwa mujibu wa kamishina wa madini kanda ya kaskazini Benjamin Mchwampaka alisema kuwa tayari kampuni hiyo imeshaanza kulipa deni hilo na kwamba hadi sasa imeshatoa malipo ya dola 200,000 zaidi ya fedha za kitanzania milioni 310,huku serikali ikiitaka kuhakikisha inamaliza kulipa deni hilo hadi kufikia jamuari mwaka 2013.

Hata hivyo katibu huyo aliitaka TAMIDA kuisaidia serikali kuyafichua makampuni yanayokwepa kulipa ushuru wa madini wakiwemo baadhi ya wafanyabiashara wakubwa ili wachukuliwe hatua na kusisitiza kuwa kwa sasa serikali imeanza mkakati wa kupitia upya mikataba ya makampuni ya madini hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hilo nchi na hilo bara la Africa ni sehemu ambayo itaibiwa hadi siku ya kihama..Africa peke yake mgeni ndio hana nguvu kuliko mwenyeji, sasa unategemea wafanyeje wakati watu ni mabwege...
    Mdau,
    Cambodia!

    ReplyDelete
  2. Hilo nchi na hilo bara la Africa litaibiwa hadi siku ya kihama, Africa peke yake mgeni ndio hana nguvu na kubabaikiwa, eti wakalimu..sasa unategemea wao wafanye nini sasa?awalipi kodi, watu mabwege tu na slow, elimu mu Africa bado haijamkomboa tunahitaji kwanza kujifunza haki zetu kwanza kabla atujakimbilia ma PHD ambayo hayana use katika uchumi mdogo kama wetu.
    Mdau,
    Cambodia.

    ReplyDelete
  3. Kwani sheria inasemaje? Mtu anayevunja vipengele vya mkataba anachukuliwa hatua gani? kwann msichukue maamuzi ya kuvunja mkataba na kutafuta kampuni nyingine tena mkitumia nafasi hii kurekebisa makosa mliyofanya kwenye mikataba mingine ya madini? kwani mmesikia hizo ni ndizi kuwa zikiachwa zitaoza? Tutoleeni ujinga wa kuja kulalamika kwa wananchi! Chukueni hatua,..

    ReplyDelete
  4. Kama hawalipi, watiwe jela, sio kufukuzwa nchini. Get priorities straight people.

    ReplyDelete
  5. Kwa kawaida deni linalipwa kwanza ndipo watimuliwe. Kama hawalipi, basi vifaa vyao vizuiwe na serikali ili viuzwe tupate fedha zetu.

    ReplyDelete
  6. Jamani hebu fikirieni sisi waajiriwa kodi inakatwa juu kwa juu lakini wengine wanakwepa kulipa na ni wawekezaji hizo pesa zitawatafuna hao wkubwa walioshirikiana nao kukwepesha hizo kodi na ndio hizo zilizoko huko Uswizi Zitto kaza buti tuko nyuma yako wataje hao na wazirudishe NA WASWEKE NDANI TUWASAHAU.

    ReplyDelete
  7. Na wale wa Uranium vipi kuhusu Capital Gain tax wanayodaiwa na TRA?

    Wasije kutokea mbavuni kwa kuuza Mgodi kwa mwekezaji mpya!

    ReplyDelete
  8. Jamani chukueni mifano ya nchi zilizoendelea yaani from 2004-2008? Shame on tanzania.Hatutakaa tuendelee.kutolipa kodi ni kosa la jinai

    ReplyDelete

  9. Halafu tunasema eti masikini!!!

    Kamua, binya hao mpaka wateme hela zetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...