Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Sued Kagasheki amebadili taratibu za kuwapata wajumbe wa Bodi mbali mbali zilozoko chini ya Wizara. Kuanzia sasa Wajumbe wa Bodi hizo watapatikana kwa njia ya ushindani badala ya kuteuliwa moja kwa moja na Waziri.
Kwa sasa kuna Bodi nane (8) ambazo muda wake umeisha au unakaribia kuisha.Bodi hizo ni za za Taasisis/Mashirika yafuatayo;-
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI)
Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI)
Makumbusho ya Taifa
Chuo cha Mafunzo na Usimamizi wa Wanyamapori (MWEKA)
Chuo cha Mafunzo ya Wanyamapori Pasiansi
Wakala wa Mbegu za Miti (TTSA)
Bodi ya Leseni za Utalii (TTLB)
Watanzania wenye sifa za kuwa Wajumbe wa Bodi hizo wanatakiwa kupeleka maombi kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.
Maelezo zaidi ya namna ya kupeka maombi yataweka kwenye magazeti na tovuti ya Wizara, www.mnrt.go.tz
NB: BOFYA HAPA KAMA UNAHITAJI KUOMBA NAFAZI ZA UJUMBE WA BODI http://www.mnrt.go.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=291:application-for-vacancies-in-the-board-of-directors-governing-body-advisory-board-licensing-board-of-some-institutions-under-the-ministry-of-natural-resources-and-tourism&catid=39:news-and-anouncements.
Hongera Mhe. Balozi Kagasheki.
ReplyDeleteHuu ndio utaratibu unaofaa hata kwa BODI ZA TAASISI ZOTE ZINGINE NCHINI.
BADALA YA KUBAKI NA UDHALIMU WA KUCHAGUANA KWA UPENDELEO TENA BILA VIGEZO VINAVYOKUBALIKA NA USHINDANI.
MATOKEO YA UTARATIBU DHALIMU WA KIZAMANI NI KUPATA WAJEUMBE WA BODI WALIOKUWA KAMA MTANDAO WA MCHEZO WA 'KARATA TATU' AMBAPO BIASHARA INAYOFUATA NI KAMA 'CHUMA ULETE' BADALA YA UENDESHAJI WA TIJA NA UWAZI.
MATOKEO YAKE JAMII INAJENGEKA KWA MATABAKA YA MABEPARI NA KUWA NA KUTA ZA WENYE NAZO NA WASIOKUWA NAZO.
CHA KUSTAAJABISHA KWA UTARATIBU WA KIZAMANI WA KUCHAGUA WAJUMBE WA BODI INASHANGAZA KUKUTA NAO WANAKUWA NI WAFANYA BIASHARA WAKUBWA NA WADAU WAKUBWA WA SEKTA HIYO HIYO HUKU WAKIJIPA UPENDELEO KTK TASNIA NZIMA.
KTK SHERIA ANUAI ZA UMILIKI WA MAKAMPUNI NA BODI ZA UENDESHAJI, KIMATAIFA ILI KUTOA INFLUENCE,DOMINANCE AND INTIMIDATIONS NA KUWATENDEA HAKI WADAU WA KAWAIDA WASIO KTK SAFU YA BODI ZA UENDESHAJI, WAJUMBE WA BODI WANATAKIWA WAWE WANAFUATA MASHARITI MKUBWA MATATU:
1.WASIWE NA NAFASI KTK BODI ZAIDI YA MOJA WAKIKAA KAMA WAJUMBE WA BODI.
2.NUSU YA WAJUMBE WA BODI WASIO KUWA WAKURUGENZI WAKUU WANATAKIWA WAWE WAKURUGENZI WANAOJITEGEMEA.
3.IDADI YA HISA ZAO NA UKUBWA WA MITAJI YAO AU MADARAKA KTK BODI UWE NA UKOMO, ILI WASIWEZE KUATHIRI MAAMUZI KWA UKUBWA WAO KTK BODI NA KUTOA FURSA SAWA KWA WADAU WA KAWAIDA.
Ahsante sana tena sana Mhe. Balozi Kagasheki kwa kuwa tumekuwa kizani kwa muda mrefu sana na mabadiliko haya ya upataji Wajumbe wa Bodi ktk Wizara ya Maliasili na Utalii yanastahili kuakisiwa pia ktk Bodi za Sekta zingine, Mashirika na Taasisi zingine.