1. Chris Cremence 100,000
2. Anonymous 500,000
3. Maggid Mjengwa 100,000
4. Raymond Kasoyaga 20,000
5.Edward Mgogo 10,000
6.Joachim Kiula 5,000
7.Libory Muhanga 5,000
8.Geofrey Kagaruki 10,000
9.Sadiki Mangesho 10,000
10. Edwin Namnauka 40,000
11.Daud Mbuba 10,000
12. Anonymous 200,000
Jumla: 1,10,000 ( Milioni Moja Na Kumi Elfu)
Kiasi kilichobaki kutimiza lengo? 1, 190,000 ( Milioni Moja Na Laki Moja Na tisini Elfu)
Kiasi kilichobaki kutimiza lengo? 1, 190,000 ( Milioni Moja Na Laki Moja Na tisini Elfu)
Background:
Ndugu zangu,
Daud Mwangosi ambaye pia alikuwa ' Mwanakijiji' mwenzetu hapa Mjengwablog hatunaye tena. Nimemfahamu Daud Mwangosi tangu mwaka 2004 nilipofika Iringa. Tangu wakati huo, amekuwa akiinipa ushirikiano mkubwa kwenye kazi ya kutangaza shughuli za kijamii kwenye Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi. Ni kwa kupiga picha za televisheni na kurusha habari kwenda Channel Ten; Iwe ni kwenda naye Ilula au Njombe, Daud Mwangosi alikuwa tayari kila nilipomwomba aongozane nami kwa shughuli ya kijamii.
Mara nyingi nilimkuta Daud ofisini kwake ( Picha ya kwanza juu) akichapa kazi na huku mkewe akimsaidia kazi nyingine. Daud Mwangosi alikuwa mbunifu. Alikuwa ni mwenye kiu ya kujifunza mambo mapya kwenye teknolojia ya habari na mawasiliano.
Najua Daud Mwangosi alikuwa na malengo ya kuendeleza shughuli zake za ujasiriamali. Mbali ya mambo mengine, alikuwa na Photocopy machine ya kumwongezea kipato ambayo iliharibika mwaka jana. Akawa na ndoto ya kuwa na studio ndogo ya kupiga picha za vipande ( Passport Size). Yote ni katika kumwongezea kipato kutunza familia yake.
Leo Daud Mwangosi hayuko nasi. Ameacha familia, mjane na watoto wanne; Itika Mwangosi ( Mjane) Nehemia Mwangosi ( 17) Kidato cha Nne Malangali Sekondari, Hetzgovina Mwangosi (12) Bathsheba Mwangosi (9) na Moria Mwangosi ( 2)
Namini Daud Mwangosi angependa shughuli alizokuwa akizifanya ziendelee na zije kuwasaidia watoto wake pia.
Jana na leo nimewasiliana na mjane wa marehemu Mwangosi ambaye bado yuko Tukuyu. Nikamwambia kuna ' Wanakijiji ' wa Mjengwablog walioguswa na msiba wa Mwangosi na wangependa kutoa pole yao imsaidie katika kupata mwanzo kutoka hapa alipo sasa. Mjane wa Mwangosi amefarijika sana kusikia habari hizo.
Kwa vile tayari ameahidiwa msaada wa kusomeshewa watoto. Msaada anaouhitaji kwa sasa ni kupata photocopy machine ( Used) na kodi ya pango la ofisi. Jumla yake kwa yote hayo mawili haitazidi shilingi za Kitanzania milioni mbili na laki mbili. Hivyo msaada anaouomba kwa wenye mapenzi mema ni shilingi 2, 200,000 ( Shilingi milioni mbili na laki mbili). Shughuli hizo zitamsaidia kujikimu.
Kutokana na hali aliyo nayo sasa, Mwenyekiti wenu napendekeza nichukue jukumu la kuratibu michango hiyo. Shime tushirikiane kufanikisha hili ili tumsitiri mjane wa mwenzetu Daud Mwangosi. Napendekeza ifikapo mwisho wa mwezi huu ( Septemba) tuwe tumefanikisha zoezi hili kwa yeyote aliye nacho, hata kama ni shilingi elfu tano, ni msaada mkubwa.
Mjengwablog bado tuna rekodi nzuri katika kuchangishana kuwasaidia wenye kuhitaji. Itakumbukwa, huko nyuma, kwa pamoja, tulifanikisha kukusanya michango ile ya watoto wa Somalia na kuikabidhi UNICEF, Dar es Salaam. Ni zaidi ya shilingi milioni mbili.
Tulifanikisha mchango wa kusaidia ukarabati wa maktaba ya Kijamii kijijini Mahango, Madibira. Zaidi ya shilingi milioni nne.
Sasa ni zamu ya kumchangia mjane wa mwenzetu Daud Mwangosi. Kinachohitajika ni milioni mbili na laki mbili.
Naam, kutoa ni moyo, usambe ni utajiri.
Mwenyekiti wenu na familia yangu naanza kwa kuchangia shilingi laki moja.
Na kama kawaida, taarifa za waliochanga na kiasi kilichopatikana kitawekwa kwenye blogu kwa kila mmoja kuona.
Namna ya kuwasilisha michango: Tumia M-Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money au NMB Mobile. Kwa namba , , ( Kwa walio nje mnaweza kutuma kwa Western Union, jina la mpokeaji- Maggid Mjengwa)
Natanguliza Shukrani.




Watanzania wenzetu, inapotokea vitu kama hivi, tuelezeni na sisi wenzenu tulioko nje ya nchi namna ya kuchangia, tupo pamoja ingawa sisi inaonekana kama vile watu ambo hawapo,lakini ukweli ni kwamba sisi tupo na tuhusisheni katika michakato mbalimbali hamna shida, sasa hivi Dunia ni kama kijiji kimoja.
ReplyDeleteTulio ughaibuni tukitaka kutuma kwa western union kazima tuwe na address ambayo itaonyesha mji na pia namba ya simu ya mtu unaemtumia, pia nikishatuma natakiwa nikupe secret answer, naomba uturahisishie, nimeguswa
ReplyDeleteMdau
Marekebisho kidogo kwenye hiyo takwimu jumla ya fedha iliyopatikana.Inasomeka ni laki moja na kumi elfu badala ya Milioni moja na kumi elfu.
ReplyDeleteWadau mlioko nje jina la mpokeaji Lipo majid mjengwa,mji aliopo iringa na cm zake kaweka,nchi tz,sasa hapo bado nini?ukituma pesa Africa unaweka swali then unampa jibu na code tu,ni wewe tu hakuna kilichokosekana.kutoa ni moyo.
ReplyDeleteyaani waandishi woote na wengine mmeshindwa kufikisha hata milioni 10.
ReplyDeletePOLISI WAMECHANGA KIASI GANI ??
ReplyDeleteHongera Majid Mjengwa. Hii bora kuliko kuchangia Sherehe za Harusi. Tuanze kuona Mbali badala ya Mbele! Na tuamke kuleta mabadiliko halisia yatakayo ongozwa na Katiba Mpyaaaa.
ReplyDeleteyaani kelele zote zile waandishi wa habari hizo ndizo mlizochanga.
ReplyDeleteUkiaka kutuma hela western union kwenye tanzania unaweza kuweka mji wowote unaitaji jina tu na umpe mtu swali la siri na namba. Ndiyo uzuri wa bongo hakuna kuzungushana, kwa wageni ukichukuwa usisahau kuacha ya chai next time utahudumiwa kama mfalme. Ila siyo siri watu wanaokaa nje wanaaibisha kila mahali wakitoa comments. Hivi huko hamuendi shule au kujielimisha. Ndenda kwenye forums ndiyo utajua nazungumzia nini.
ReplyDeletekaka majid mjengwa ubarikiwe sana kwa moyo ulionyesha wa kujali familia ya marehemu. Angalia kusiwe na wakuu wa familia ya marehemu wenye mawazo tofauti unajua familia za kiafrika wanandugu wakijua kuna mapesa yanachangwa wakaingilia usimamizi wa mali za marehemu na kibao kikageuka kwa mjane na watoto wake naomba ulifatilie hilo kwa ukaribu sana wewe kama mmoja watu wa karibu na marehemu saidia mjane ajipange kisawasawa asiingiliwe na mila zetu potofu, msiba huu unauma sana poleni wanafamilia
ReplyDeleteOhh my God ndo hivyo na serikali imekaa kimya, pole mama, ninaumia sana nikiifikiria Tz, hivi kweli tunalindwa na serikali au cc ndo tunailinda serikali? Pia ushauri mwingine tuwe tunawapa watu moyo kama mtu mzuri anasaidia Jamii basi aambiwe kabla hajafa ili hata cku zake zikiisha hapa duniani awe anajua aliowaacha walikuwaje kwake
ReplyDeletechangeni hela acheni kiswahili kirefu hapa
ReplyDeleteKama sitakuwa nimekosea, milioni moja na elfu kumi kwa tarakimu inaandikwa hivi 1,010,000/= na sio 1,10,000/=.
ReplyDeleteTuache utamaduni mbaya wa kuchangia Harusi badala yake tuchange kwa madhila kama haya, huku tukimtanguliza Marehemu David Mwangozi mbele za Haki kwa Mwenyezi Mungu, ili tuweze kumjali Mfiwa aliyeachwa nyuma na malezi ya watoto.
ReplyDelete