Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kabla ya kikao cha NEC, leo mjini Dodoma. Wengine, waliokaa. Kutoka kushoto ni Mawaziri Wakuu wa zamani, John Malecela na Cleopa Msuya, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Sheni, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na Kulia ni Mawaziri wakuu wa zamani Frederick Sumaye na Edward Lowassa.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifuatana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Sheni baada ya kuwasili Chama, alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wana-CCM, alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mjini Dodoma leo.
Baadhi ya wajumbe wa NEC wakiwa ukumbini kwenye kikao cha NEC mjini Dodoma leo.Picha na Bashir Nkoromo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Why do I see old faces with the usual suspects when I look at CCM leaders. Are their ideas as old as they look? Is it time for a new blood people.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...