Kutoka kulia..Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Ndugu Martine Shigela akichangia ajenda katika kikao cha Baraza la Umoja huo,(katikati) ni Makamu Mwenyekiti Ndugu Beno Malisa na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Mfaume kizigo, wakiwa katika kikao cha Baraza hilo kililofanyika Jana tarehe 12 katika ukumbi wa sekretarieti maarufu kama (white house) uliopo Makao Makuu ya Chama, Dodoma.
 Baadhi ya maafisa na watendaji wa Umoja wa Vijana,Wa kwanza kushoto Ndugu Shara Ahmed (Mkuu wa Kitengo Cha Oganaizesheni Unguja) Ndugu John Milele (Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uchumi) Ndugu Deogratius Daffi (Mhasibu Mkuu) na Ndugu Salmin Dauda(mwenye laptop) Mkuu wa Kitengo Cha Benki ya Vijana)
 Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)  katika mjadala wa kupitisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya Umoja huo ngazi ya Mkoa na Taifa.
 Mjumbe wa Baraza la vijana (UVCCM) ambae pia ni Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Pwani na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mheshimiwa Abdalah Ulega akichangia jambo katika Kikao hicho kilichofanyika jana katika ukumbi wa Sekretarieti, Dodoma.

Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)  wakifuatilia hoja kutoka kwa mmoja miongoni mwa wajumbe katika mjadala wa kupitisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya Umoja huo ngazi ya Mkoa na Taifa.

Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kweli tatizo la Utawala wa juu ni kuwapa madaraka watu kwa kufahamiana na sio utendaji wao!

    M/Kiti wa umoja huu mkoa wa Pwani ambae pia kwa sasa ni Mkuu wa wilaya ya Kilwa! Mh! Mh!

    ReplyDelete
  2. kabla hamjaenda kuvamia matatizo ya vyama vingine mngetumia muda wenu kutatua matatizo yenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...