Wazanzibari wanaoishi Canada ambao wanajumuika pamoja chini ya Jumuia yao
ijulikanayo kama ZACADIA (Zanzibar-Canadian Diaspora Association)
wameshitushwa na kusikitishwa na hali ya kiafya ya mtoto Nairat na dada yake
pamoja na familia yao nzima kwa ujumla - kama walivyosoma huko nyuma kwenye
ukumbi wa ZANZIBAR NI KWETU < http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2012/08/please-help-this-kid-mtoto-nairat-seven.html>.
Kutokana na hali hio mbaya ya kiafya ya
watoto, ZACADIA katika kusaidia matibabu ya Nairat na dada yake inatoa mchango wake wa TShs 750,014.04
Pesa hizo zimepelekwa Zanzibar leo tarehe 21
September, 2012 kutoka Canada kwa njia ya MONEYGRAM, kupitia kwa Bi Salma Said ambae ni mdhamini wa hawa
watoto kwa hivi sasa.
Kwa niaba ya Wana-Zacadia wote waishio Canada
tunamtakia mtoto Nairat pamoja na dada yake shifaa ya haraka na kwa wakati huo
huo tunaitakia Zanzibar kila mafanikio katika wakati huu mgumu wa kiuchumi kwa
Ulimwengu mzima.
Kila la kheri.
Hassan Othman
Katibu / ZACADIA (Toronto, Canada).


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...