Redds miss kanda ya temeke Edda Sylivester katikati akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Catherine Masumbigana kushoto na Flaviana Maeda kulia mara walipotangazwa kuwa Redds Miss Kanda ya Temeke kwenye fainali iliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA Hall usiku wa kuamkia Leo Picha zote kwa Hisani ya Intellectuals Communications Limited.
Katika shindano hilo washehereshaji walikuwa wasanii wanaong’ara katika luninga, Mpoki wa kundi la Komed Original na Steve Nyerere ambao walionekana kuvunja mbavu za mashabiki waliyoudhulia shindano hilo. Licha ya kuwepo kwa Mpoki na Steven Nyerere Bendi ya muziki Mashujaa Wanakibega ambao waliweza kutoa burudani ya nguvu chini ya Rais wao Charles Baba.
Taji la Redd's Miss Temeke, linashikiliwa na mrembo Husna Twalib. Warembo wa Miss Temeke wamekuwa wakijifua kwa wiki tatu sasa chini ya ukufunzi wa Leyla Bhanji, ambaye amekuwa akisaidiwa pia na warembo wa miaka ya nyuma wa Miss Temeke akiwemo, Regina Mosha(2002, Hawa Ismail(2003).
Washiriki wa mwaka jana Joyce Maweda, Mwajabu Juma, Cynthia Kimasha na katika shoo wamekuwa na Dickson Daud kutoka kundi la THT.
Mbali ya Redd's, Miss Temeke 2012 pia imedhaminiwa na City Sports Lounge, Jambo Leo, Mariedo Boutique, Global Publishers, Dodoma Wine, Push Mobile, Mariedo Boutique, 100.5 Times FM, Kitwe General Traders, Fredito Entertainment, katejoshy.blogsport.com na 88.4 Cloud's FM.
Temeke imewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mara tatu, kupitia warembo Happiness Sosthenes Magesse aka Millen mwaka 2001, Sylvia Remmy Baham mwaka 2003 na Genevieve Mpangala. Lakini pia imetoa warembo waliowahi kushika nafasi ya pili na tano bora katika Miss Tanzania kama Jokate Mwegelo, Irene Uwoya, Irene Kiwia, Queen David, Cecylia Assey, Sabrina Slim, Miriam Odemba, Ediltruda Kalikawe na Asela Magaka.
Tanp Bora
Redds miss kanda ya temeke Edda Sylivester katikati akifurahia ushindi pamoja na mshindi wa pili Catherine Masumbigana kushoto na Flaviana Maeda kulia


picha hazionekani
ReplyDeletePicha hazionekani!!! miminilidhani ni hapa kwangu tu!!!
ReplyDelete