Na Profesa Mbele



Tamasha la vitabu liitwalo Twin Cities Book Festival litafanyika tarehe 13 Oktoba mjini St. Paul, Minnesota. Litafanyika kwenye sehemu maarufu iitwayo State Fairgrounds. Hii ni mara ya kwanza kwa tamasha hili kufanyika nje ya mji jirani wa Minneapolis. Nimeshiriki tamasha hili kwa miaka kadhaa, kama nilivyoelezea hapa na hapa.

Mimi kama mwandishi wa vitabu nimeshalipia meza. Hapa pichani ni vitabu vyangu nitakavyopeleka kwenye tamasha. Sasa nangojea tu siku ije, nikajumuike na wadau mbali mbali katika nyanja za uandishi, uchapishaji, uuzaji, na uchambuzi wa vitabu.  Nangojea kuwashuhudia tena maelfu ya watu wa hapa wakiwa katika heka heka za kuangalia vitabu, kuvinunua, kuongea na waandishi, wachapishaji, wauza vitabu, na kadhalika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...