Mkurugenzi katika Ofisi ya Spika Ndg. Daniel Eliufoo akifuatilia kwa makini mada kuhusu “The Politics of Constitution-Making, the Role of Parliaments in Relation to the People” wakati wa warsha mbalimbali zilzoandiliwa kwa wajumbe wa Mkutano wa 58 wa CPA Mjini Colombo Sri Lanka.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu akishiriki katika warsha iitwayo “Ensuring Adequate Parliamentary Scrutiny of Foreign and Commonwealth Affairs” wakati wa Mkutano 58 wa CPA Mjini Colombo Sri Lanka. Mhe Zungu alishiriki na warsha nyingine iitwayo Terrorism - The Threat to Democracy, Peace and Security.
Mhe. Zitto Kabwe alikishiriki katika warsha iitwayo “Tackling Youth Unemployment” wakati wa Mkutano huo mjini Colombo, Sri Lanka
Mjumbe mwingine kutoka Tanzania Mhe. Rashid Mohamed akishiriki katika warsha ya “Should the Commonwealth Establish a Commissioner for Democracy, the Rule of Law and Human Rights”
Picha zote na Owen Mwandumbya
Colombo Sri Lanka,
Ili kuhakikisha kuwa kila Mjadala na warsha zinazofanyika katika mkutano wa 58 wa CPA hapa Mjini Colombo, Ujumbe wa Tanzania umejigawa katika makundi kuhakikisha kuwa kila warsha ina uwakilishi wa Tanzania. Hatua hii imesaidia kuweza kupata michango mbalimbali ikiwa ni pamoja na uzoefu wa nchi nyingine za jumuiya ya madola katika kushughulikia maswala mbalimbali ya Kidunia. Akishiriki katika warsha iitwayo "“Engaging Political Parties to improve gender – responsive Governance” Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda ameelezea uzoefu wa Tanzania katika kuwawezesha wanawake katika ngazi za Maamuzi.
Akitoa Mfano kwa Wabunge wa Viti Maalum, Mhe. Makinda amesema utaratibu huu ni wakikatiba Tanzania ambapo kwa kiasi kikubwa umewawezesha wanawake wengi kuweza kuwa wabunge wamajimbo baada ya kupata uzoefu kupitia viti maalum. Amesema wabunge wengi wa majimbo Tanzania walianza kupitia viti maalum na wakaonekana kuwa wanaweza na hvyo kukubalika na wananchi na hivi sasa ni wabunge wa Majimbo.
Kwa upande wa Uongozi katika serikali, Mhe. Makinda ameilezea Tanzania kuwa kama mfano wa kuigwa katika nchi nyingine ambapo Serikali iliyopo madarakani hususani Mhe. Rais ameweza kuteuwa idadi kubwa ya Majaji wanawake ikiwa ni pamoja na watendaji mbalimbali katika ngazi ya kitaifa na hata halmashauri.
Ujumbe wa Tanzania ulijigawa katika warsha nyingine ambapo Mhe. Mussa Azzani Zungu alishirki katika warsha kuhusu “Ensuring Adequate Parliamentary Scrutiny of Foreign and Commonwealth Affairs” na warsha nyingine iitwayo Terrorism - The Threat to Democracy, Peace and Security. Mhe. Zitto Kabwe alikishiriki katika warsha iitwayo “Tackling Youth Unemployment” ambapo Mjumbe mwingine kutoka Tanzania Mhe. Rashid Mohamed akishiriki katika warsha iitwayo “Should the Commonwealth Establish a Commissioner for Democracy, the Rule of Law and Human Rights?”. Mkutano huo wa 58 wa CPA ulianza tarehe 7 na unatarajiwa kumalizika tarehe 15 September, 2012. Tanzania ilipata nafasi ya kuandaa mkutano wa namna hii mwaka 2009 ambapo ulifanyika Mjini Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...