Mkurugenzi wa Lino Agency ambao ni waandaaji wa Mashindano ya Redd's Miss Tanzania,Hashim Lundenga (pili Kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari kwa Msisitizo kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati wa kutangaza kuanza kwa kambi rasmi ya Redd's Miss Tanzania 2012 na ukumbi utakaofanyiwa Shindano hilo mwaka huu ambao ni Blue Peal uliopo ndani ya Jengo la Ubungo Plaza,jijini Dar es Salaam.Jumla ya Warembo 30 wataingia kambini Oktoba 2 kwenye hoteli ya Girrafe jijini Dar es Salaam.Wengine Pichani toka kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Redd's Original,Victoria Kimar,Miss Tanzania 2011,Salha Israel pamoja na Mshindi wa Nne wa Miss Tanzania 2011,Jennifer Kakolaki.
Meneja wa Kinywaji cha Redds Original,Victoria Kimaro akiongea mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi walivyojipanga wakiwa kama wadhamini wakuu wa Shindano hilo la Redd's Miss Tanzania 2012.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa katika mkutano huo uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo,jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Jamani Mbona Lundenga hataki kuachia ngazi hawezi fanya lolote tena na UMRI umempotea!

    Achia vijana Lundenga wewe sasa umepitwa na wakati.

    ReplyDelete
  2. Lundenga! Lundenga! Umri kaka na hii biashara hapana tena! achia vijana wadogo wabunufu!

    ReplyDelete

  3. Acheni hizo, nyie mmeacha mangapi? Hiyo ni biashara bro anafanya, hawezi kusema anatengeneza ngapi.

    Aache biashara? Kama ndio inayomuingizia?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...