Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Oman katika mtaa wa balozi jijini Muscat Oman jana.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe, (watatu kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Oman, Ali Ahmed Saleh na (kulia) ni Afisa Mwandamizi Ubalozi wa Tanzania nchini Oman, Bwana Abdallah Kilima.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizindua ujenzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Oman jana.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe,watatu kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Oman, Bw. Ali Ahmed Saleh, (wanne kulia aliyeshika karai) ni Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Oman, Bw. Abdallah Kilima na (kulia anayeshuhudia) ni Afisa katika Ubalozi huo, Bw. Saidi Mussa.Picha na Freddy Maro-IKULU
Serikali ya
kifalme ya Oman inatarajia kutuma ujumbe wake ambao utajumuisha
na wafanyabiashara kuja Tanzania kutathmini na
kuangalia maeneo gani nchi hiyo na wafanyabiashara wake wanaweza kuwekeza ,
kufuatia ziara ya kiserikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete ya siku 4
nchini Oman.
"Tutaunda
kamati na kutuma ujumbe kwenda Tanzania kuangalia na kujua aina gani ya
biashara na vitega uchumi Oman inaweza kuwekeza”.Amesema Naibu Waziri
Mkuu wa serikali ya kifalme ya Oman, Mheshimiwa Sayyid Fahad Mahmood Al Said
wakati wa mazungumzo yao ya kiserikali.
Naibu Waziri
Mkuu huyo amesema Oman ina matumaini makubwa kuhusu mazungumzo yao ya tarehe 17
Octoba, 2012 yaliyofanyika katika makao makuu ya Baraza la Mawaziri.
Amesema Baraza
la Mawaziri la nchi yake litakaa na kujadiliana pamoja na Chama cha
wafanyibiashara na Viwanda kuandaa serikali ya kuja Tanzania na kuhakimisha
mahusiano yetu yanadumu.
Rais
amemueleza Makamu wa Waziri Mkuu kuwa Tanzania hivi karibuni imegundua gesi kwa
wingi na hivyo kuna changamoto kubwa ya kujenga uwezo kwa watu wake waweze
kujadiliana na kuwekeana mikataba itakayoleta tija kwa Taifa na watu wake.
Rais Kikwete
pia amekutana na watanzania wanaoishi na kufanya kazi nchini Oman ambapo
amewaeleza kwa kifupi maendeleo yanayoletwa na serikali katika Nyanja za
Kilimo, Elimu, Afya, miundombinu na mambo mbalimbali ya kisiasa yanayoendelea
nchini Tanzania.
Watanzania hao
, nao wamepata nafasi ya kuelezea matatizo na matarajio yao kwa Rais , ambapo
Rais amewapata nafasi ya kufafanua na kujibu baadhi ya hoja zao na kuwapa
changamoto watanzania wote wanaoishi nchi za nje ya kushiriki katika
shughuli za maendeleo na kukuza Uchumi wa Tanzania kwa kutafuta na
kushawishi wawekezaji na marafiki mbalimbali kusaidia katika nyanja mbalimbali
ambazo zinahitaji misaada ya maendeleo.
Rais anamaliza ziara yake tarehe 18 Octoba, 2012 na kurejea nyumbani
jioni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...