Meneja wa Sekta Kupunguza Umaskini na Kusimamia Maendeleo ukanda wa Afrika wa Benki ya Dunia Dkt Albert Zeufack, akongea wakati wa mkutano na wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam leo kuhusu sekta ya Gesi asilia nchini, akiwa ameongozana na mabalozi wa nchi kadhaa pamoja na Timu ya wataalam walioletwa na washirika wa maendeleo na inayowakilisha Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa, Jumuiya ya Nchi za Ulaya na Nchi za China, Uingereza na Ujerumani
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akongea wakati wa mkutano na wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam leo kuhusu sekta ya Gesi asilia nchini. Nyuma yake mwenye laptop ni Meneja wa Sekta Kupunguza Umaskini na Kusimamia Maendeleo ukanda wa Afrika wa Benki ya Dunia Dkt Albert Zeufack, akiwa ameongozana na mabalozi wa nchi kadhaa pamoja na Timu ya wataalam walioletwa na washirika wa maendeleo na inayowakilisha Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa, Jumuiya ya Nchi za Ulaya na Nchi za China, Uingereza na Ujerumani
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya waandishi wa habari baada ya mkutano na wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam leo kuhusu sekta ya Gesi asilia nchini.Mkutano huo ulihudhruiwa pia na mabalozi wa nchi kadhaa pamoja na timu ya wataalam walioletwa na washirika wa maendeleo na inayowakilisha Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa, Jumuiya ya Nchi za Ulaya na Nchi za China, Uingereza na Ujerumani ilipotembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo. Wa pili kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Bw. Mathias Chikawe, akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzan Mlawi na maafisa waandamizi wa Ofisi ya Rais, kamati hiyo.
BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI
BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI





habari zenu wote..najua si muda muafaka na wala si mahala pake lakini kuna jambo limekuwa likinisumbua akili yangu, mustakabali wa taifa letu..nasema hivyo kwa kuzingatia kwamba kila mmoja wetu anatambua mambo ya kijamii,kiuchumi na kisiasa yanayoendelea hapa nchini kwetu..kutokana na kasumba ambayo imeendekezwa na wanaotuongoza kama taifa kwamba kiongozi mkuu au mwandamizi lazima atoke miongoni mwao(cabinet au wabunge au nec members) na kwakuwa wanatumia muda mwingi kujitengenezea mazingira ya kupata urahisi wa kupata nafasi hizi nyeti..kwanini sisi walengwa(watanzania) tusifanye mchakato wetu wenyewe wa kusource mtu anayetufaa kuwa kiongozi wetu bila kusubiri cuf,chadema na ccm kutuacha bila chaguo halisi kwa kutuletea mtu wao ambaye ataserve interest ya nec members(ndo maana baadhi yao wanataka hata kuuana ili wapate nafasi ya kutuchagulia mgombea kwani wanajua reward yake). sitaki kuwa mtanzania anayelalamika na kusubiri wengine wanitatulie matatizo yangu.. mimi naanzisha mchakato sasa na wazo langu limenifanya nimwone katibu mkuu kiongoz, mr OMBENI SEFUE kama mtu anayefaa kuwa kiongozi mkuu anayetufaa baada ya kiongozi aliyepo kumaliza muda wake. naomba niwe wazi,huyu jamaa sina undugu naye na wala sijui kabila lake wala dini yake ila nafahamu ni mtu mwenye uwezo wa kuchanganua mambo na anaweza kutengeneza team ya kuwaletea watanzania maendeleo ya dhati...OMBENI SEFUE FOR PRESIDENCY.
ReplyDelete