Katika kipindi cha Miaka kadhaa iliyopita,ilikuwa ni fahari sana kuwaona Kunguru hawa wa mabaka meupe katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar na Tanzania nzima kwa ujumla kwani walikuwa ni wasafishaji wazuri sana wa jiji letu hili na wastaarabu.lakini walipotia timu wale wengine wa kutoka kule nanihii ambao ni washari na ni wachafu kupitiliza na wadokozi waliokubuhu,waliwakimbiza kabisa kunguru hawa wa mabaka meupe na kukaa wao ambao ustaarabu kwao ni sifuri.Maana unaweza jikuta siku umekaa kwa mama ntilie unapiga zako msosi,unamuona anakuja na kuanza kukuzonga na ikiwezekana hata kukukwapulia bakuli ya mboga.yaani wanakera kama nini vileee.
Hebu angalia hawa walivyo wapole,yaani hadi unavutika kuendelea kuwaangalia.





hawa walikuwa wajasiriamali zaidi. hawa wa sasa wamekaa kifisadi fisadi...
ReplyDeleteNini kukwapua mboga, kwa kulenga hao ni balaa. Maana unaweza kupigilia kaunda suti yako unaelekea kanisani kama leo j2, mara fyaa! kesha kuachia uharo!
ReplyDeletehawa kunguru waliokuwa wadokozi wa sabuni za vipande nakumbuka nilipokuwa mdogo nilikuwa naishi mkoa wa mbeya na hawa kunguru wenye mabaka meupe ndo waliopo mbeya basi ukiacha kipande cha sabuni njee hukikutii, wadokozi wanyama, samaki, vifaranga vya kuku, vitoto vya paka hawaa mmoja wao akiuna kitu basi ataaawaita wenzie wotee
ReplyDeleteHawa jamaa wavaao vizibao vyeupe walikuwa wastaarabu kidogo kuliko ndugu zao ambao ni wahuni, wizi wagomvi na wana fujo na makelele.Nilishuhudia kule pwani Zbar hao kunguru wasio na vizibao walipomwibia mvuvi pochi lake na fedha zote za kazi ya siku nzima, jamaa alilia kama mtoto.
ReplyDeleteNadhani katika uumbaji wake MOLA tukumbuke, katika kila kitu au kila tabia kaviumba viwili viwili na hata kinyume chake, mfano kuna mazuri/mabaya, mkubwa/mdogo, msafi/mchafu, kulia/kushoto n.k. Basi hata hawa kunguru tunaoendelea kuwatia ila hizi na zile, nadhani ndio jumla ya utofauti huo. Tunaopoendelea kuwapigia kelele, kwanza tungekitafuta chanzo na sababu zao za kuwakimbiza hao wapole mpaka wakatoweka wote. MaanaTulivyowaandama utadhani tunawananga kunguru watu, haiwi binaadamu anahana toka sehemu moja kwenda nyingine huku akiwa sambamba na silka zake tofauti nzuri na mbaya kuliko hata za hao Kunguru, lakini hayo hatuyaoni, hebu tuwaache Kunguru weusi tusiwasakame bure, nao pia ni viumbe na hizo ndio jumla ya silka zao, khalaaaaas!
ReplyDeleteKunguru mstaarabu na mtanashati anaitwa Common Magpie aka Pica pica, close relatives are Pied crow aka Corvus albus and Australian magpie aka Gymnorrhina tibecen, Kunguru wa zali mgomvi na kibaka sugu yeye anaitwa Indian house crow aka corvus splendes, ndugu zake wa karibu ni Common Raven aka Corvus corax, Rook aka Corvus frugilegus na Carrion Crow aka Corvus corone
ReplyDeleteNgege mwenye akili nyingi!
ReplyDeleteKunguru weusi walitokea Zanzibar!
ReplyDeleteHii shari na fujo ndio ule ustaarabu uliokosekana kwa baadhi ya wakazi wa Huko Visiwani hasa ktk Medani ya Siasa ambao wameulete Bara hawa Kunguru!