Wizara ya Maliasili na Utalii itaendesha zoezi la kuwaangamiza
kunguru weusi katika mikoa ya Tanga na Pwani kuanzia tarehe 2 Oktoba hadi 1 Novemba 2012 kwa kutumia sumu tulivu
aina ya DRC 1339.
Zoezi hilo limehamia katika mikoa hiyo baada ya kukamilika mkoani
Dar es Salaam ambako liliendeshwa kwa mwezi mzima tangu tarehe 27 Agosti 2012
hadi 25 Septemba 2012. Katika zoezi hilo jumla ya kunguru 41,487 waliuwawa
Jijini Dar es Salaam.
Aidha, tangu
Mradi wa kudhibiti kunguru weusi uanze Mwezi Julai 2010, hadi Septemba 2012
jumla ya kunguru weusi 807,961 wameshauawa kwa kutumia sumu hiyo ya DRC 1339 na
mitego katika Mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Pwani na Tanga.
Ingawaje sumu hiyo haina madhara makubwa kwa binadamu, wananchi hasa
watoto, wanatakiwa kutochezea mizoga ya kunguru ambao watakuwa wamekufa
kutokana na sumu hiyo. Endapo mtu atakuwa ameishika mizoga hiyo anatakiwa anawe
kwa sabuni.
Kunguru weusi
wanauwawa kwa lengo la kupunguza idadi yao ili wasiendelee kusababisha kero kwa
wananchi kwa kupokonya chakula na vitu mbalimbali. Aidha, kunguru wamekuwa wakieneza
vimelea vya magonjwa mbalimbali kwa binadamu na kuku.
Wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa vikosi ambavyo vitakuwa
vinaokota mizoga ya kunguru, kwa kuonyesha iliko. Pia wanatakiwa kutoa taarifa
pale watapogundua kuwa kuna idadi kubwa ya ndege hao sehemu yoyote ili hatua za
kuwaangamiza ziweze kuchukuliwa.
Taarifa zipelekwe katika ofisi za
Maliasili za Mikoa, Wilaya, na Manispaa. Pia wanaweza kupiga simu 0716 129120 kwa Mkoa wa Pwani na 0757 585358 kwa
Mkoa wa Tanga.
Zoezi la kuwaangamiza kunguru weusi
litahamia mkoani Morogoro tangu tarehe 5 Novemba 2012 ambako litaendeshwa kwa
muda wa mwezi mzima. Baada ya kumalizika kwa zoezi katika mkoa huo Wizara
itafanya tathmini ili kuona mafanikio ya operesheni hii. Tathmini katika mikoa
yote minne (Dar es Salaam, Pwani, Tanga, na Morogoro) itafanyika kwa pamoja kwa
kuwa kunguru wanaoonekana katika mkoa mmoja ndiyo walewale ambao huzungukia
mikoa yote inayopakana nao.
George
Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
1 Oktoba
2012
Simu : +255 784 468047
If only this commitment of eradicating these birds could be transfer to a commitment of eradicating corrupted leaders in all elements of the society would be wonderful ;)
ReplyDeleteHehnehehe First Mdau the plane is now taking off after the final KUNGURU DEATH,,,,,,THEN WE WILL TRANSFER TO CORRUPT AND GRAFT LEADERS SO THAT MAKE TANZANIA TOTALLY A FINE PLACE TO LIVE OUT OF WALA RUSHSWA, MAFISADI AND MAKUNGURU WEUSI!
ReplyDeleteHogera Wizara ya Maliasili,
ReplyDeleteMauaji ya kunguru LAKI NANE NA USHEE hadi sasa si mchezo!
Mkimaliza mrudi kwa Majangili, kama mnavyoona tumebakiwa uchache wa kutisha kama:
-Idadi ya Faru watato (5) nchi nzima tena kwa kusaidiwa kwa msaada ya mnegu kutoka Uningereza!
-Tembo wanahesabika nchi nzima!
-Twiga wanapandishwa madege usiku kwa kupindishwa shingo na kutoroshwa nje!
-Imefikia hali ya kutisha kabisa hadi mamba na majoka yanatoroshwa nje,
Sio rahisi mnyama mtata kama mamba au nyoka mkubwa chatu ukamkunja kumtia katika sanduku na kumtorosha!
Hivi watoroshaji wanatumia uchawi?
i will miss black kunguru very much
ReplyDeletenakumbuka nilipokuwa mdogo mpaka nakuwa kijana pale mitaa ya kariakoo tulikuwa kila nyumba mbili au tatu hatukosi mti mbele ya nyumba au uwani
kunguru weusi walikuwa wakirukaruka na kutoa sauti zao sauti iliyonifanya nijiosikie nipo mjini kwenye nchi ya amani
nakumbuka ilikuwa anapokufa kunguru mmoja kwa kupigwa shoti na waya wa umeme basi kunguru wengine wanajaa na kukaa kimajonzi sana kwenye msiba wa mmoja wao huyo
i will always miss you black kunguru.
mdau uholanzi.
Baada ya kuwamaliza Kunguru weusi wooote, tuwageukie Mafisadi!
ReplyDelete