Wizara ya Maliasili na Utalii itaendesha zoezi la kuwaangamiza kunguru weusi katika mikoa ya Tanga na Pwani kuanzia tarehe 2 Oktoba  hadi 1 Novemba 2012 kwa kutumia sumu tulivu aina ya DRC 1339.
Zoezi hilo limehamia katika mikoa hiyo baada ya kukamilika mkoani Dar es Salaam ambako liliendeshwa kwa mwezi mzima tangu tarehe 27 Agosti 2012 hadi 25 Septemba 2012. Katika zoezi hilo jumla ya kunguru 41,487 waliuwawa Jijini Dar es Salaam.
Aidha, tangu Mradi wa kudhibiti kunguru weusi uanze Mwezi Julai 2010, hadi Septemba 2012 jumla ya kunguru weusi 807,961 wameshauawa kwa kutumia sumu hiyo ya DRC 1339 na mitego katika Mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Pwani na Tanga.
Ingawaje sumu hiyo haina madhara makubwa kwa binadamu, wananchi hasa watoto, wanatakiwa kutochezea mizoga ya kunguru ambao watakuwa wamekufa kutokana na sumu hiyo. Endapo mtu atakuwa ameishika mizoga hiyo anatakiwa anawe kwa  sabuni.
Kunguru weusi wanauwawa kwa lengo la kupunguza idadi yao ili wasiendelee kusababisha kero kwa wananchi kwa kupokonya chakula na vitu mbalimbali. Aidha, kunguru wamekuwa wakieneza vimelea vya magonjwa mbalimbali kwa binadamu na kuku.
Wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa vikosi ambavyo vitakuwa vinaokota mizoga ya kunguru, kwa kuonyesha iliko. Pia wanatakiwa kutoa taarifa pale watapogundua kuwa kuna idadi kubwa ya ndege hao sehemu yoyote ili hatua za kuwaangamiza ziweze kuchukuliwa.
Taarifa zipelekwe katika ofisi za Maliasili za Mikoa, Wilaya, na Manispaa. Pia wanaweza kupiga simu 0716 129120 kwa Mkoa wa Pwani na 0757 585358 kwa Mkoa wa Tanga.
Zoezi la kuwaangamiza kunguru weusi litahamia mkoani Morogoro tangu tarehe 5 Novemba 2012 ambako litaendeshwa kwa muda wa mwezi mzima. Baada ya kumalizika kwa zoezi katika mkoa huo Wizara itafanya tathmini ili kuona mafanikio ya operesheni hii. Tathmini katika mikoa yote minne (Dar es Salaam, Pwani, Tanga, na Morogoro) itafanyika kwa pamoja kwa kuwa kunguru wanaoonekana katika mkoa mmoja ndiyo walewale ambao huzungukia mikoa yote inayopakana nao.

George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
1 Oktoba 2012
                                                             Simu : +255 784 468047

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. If only this commitment of eradicating these birds could be transfer to a commitment of eradicating corrupted leaders in all elements of the society would be wonderful ;)

    ReplyDelete
  2. Hehnehehe First Mdau the plane is now taking off after the final KUNGURU DEATH,,,,,,THEN WE WILL TRANSFER TO CORRUPT AND GRAFT LEADERS SO THAT MAKE TANZANIA TOTALLY A FINE PLACE TO LIVE OUT OF WALA RUSHSWA, MAFISADI AND MAKUNGURU WEUSI!

    ReplyDelete
  3. Hogera Wizara ya Maliasili,

    Mauaji ya kunguru LAKI NANE NA USHEE hadi sasa si mchezo!

    Mkimaliza mrudi kwa Majangili, kama mnavyoona tumebakiwa uchache wa kutisha kama:

    -Idadi ya Faru watato (5) nchi nzima tena kwa kusaidiwa kwa msaada ya mnegu kutoka Uningereza!

    -Tembo wanahesabika nchi nzima!

    -Twiga wanapandishwa madege usiku kwa kupindishwa shingo na kutoroshwa nje!

    -Imefikia hali ya kutisha kabisa hadi mamba na majoka yanatoroshwa nje,

    Sio rahisi mnyama mtata kama mamba au nyoka mkubwa chatu ukamkunja kumtia katika sanduku na kumtorosha!

    Hivi watoroshaji wanatumia uchawi?

    ReplyDelete
  4. i will miss black kunguru very much

    nakumbuka nilipokuwa mdogo mpaka nakuwa kijana pale mitaa ya kariakoo tulikuwa kila nyumba mbili au tatu hatukosi mti mbele ya nyumba au uwani

    kunguru weusi walikuwa wakirukaruka na kutoa sauti zao sauti iliyonifanya nijiosikie nipo mjini kwenye nchi ya amani

    nakumbuka ilikuwa anapokufa kunguru mmoja kwa kupigwa shoti na waya wa umeme basi kunguru wengine wanajaa na kukaa kimajonzi sana kwenye msiba wa mmoja wao huyo

    i will always miss you black kunguru.

    mdau uholanzi.

    ReplyDelete
  5. Baada ya kuwamaliza Kunguru weusi wooote, tuwageukie Mafisadi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...