Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi -Zanzibar

Maafisa wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama hapa nchini pamoja na Mamkala ya Bandari Zanzibar, wamefanya oparesheni maalum ya ukaguzi wa meli ya AZAM Sealink -1 iliyoingia nchini juzi kuangalia kama ina ubora na kukidhi vigezo vya usafirishaji wa abiria na mizigo majini yakiwemo magari.
 
Maafisa waliofanya ukaguzi huo ni kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Usalama wa taifa, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Mamlaka ya Usalama Bandarini na Huduma za Meli Zanzibar (ZMA) na Mamlaka ya Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA).
Pamoja na kuangalia ubora na vigezo vingine, Maafisa hao pia wamepata maelezo toshelezi juu ya ubora wa meli hiyo kutoka kwa Kampuni ya RFI iliyopewa dhamana ya kuisafirisha Meli hiyo kutoka nchini Ugiriki hadi hapa nchini.
Akizungumza na Ujumbe huo ndani ya Meli hiyo iliyoweka nanga nje kidogo ya Bandari ya Zanzibar, Mkurugenzi wa RFI Bw. Stefan Nedkoff, alisema kuwa meli hiyo imeweza kusafiri yenyewe kutoka nchini Ubeligiji hadi hapa nchini pasipo msaada wowote wa kiufundi.
Amesema kuwa katika maeneo waliyopitia walipambana na kila aina ya dharuba na kuvuka vikwazo vya mikondo mikubwa ya bahari kwenye kina kirefu na Meli hiyo iliweza kuhimili hali hiyo.
Alisema Meli hiyo inayoongozwa kwa mifumo ya kompyuta, ina uwezo mkubwa wa kuhimili misukosuko ya hali ya bahari na kusafiri umbali na kina kirefu cha maji baharini pasipo shaka.
Bw. Nedkoff amesema kuwa, mbali ya kuwa meli hiyo ilisafiri ikiwa tupu, lakini itahimili vishindo zaidi vya baharini pale itakapokuwa na abiria na mizigo ya kutosha.
Amesema kuwa mbali ya uwezo wake wa kubeba abiria 1,500, lakini pia meli hiyo inauwezo wa kuchukua mizigo yakiwemo magari 200 kutoka eneo moja kwenda jingine vyote vikiwa na uzito wa tani 500 bila ya kuwa na tatizo lolote la kiusalama.
Maafisa walioitembelea meli hiyo, wameonyeshwa njia maalum za kujiokolea pamoja na vifaa muhimu vya kiusalama vinavyoweza kutumika kwa uokozi wakati  itokeapo ajali majini.
Meli hiyo pia ina vitanda vya kutosha kwa ajili ya wagonjwa na abiria watakaojisikia kupumzika wakati wanapokuwa safarini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Zanzibar mara baada ya kuwasili kwa Meli hiyo, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Coastal Ferry inayomiliki Boti ziendazo kasi za Kilimanjaro, Bw. Hussein Mohammed Saidi, alisema meli hiyo itafanya safari zake kati ya Dar es Salaam, Zanzibar na Pemba.
Amesema Kampuni yake ambayo ipo kihuduma zaidi, pia itaangalia uwezekano wa kuweka viwango vya nauli itakayomfanya kila mtu kusafiri yeye pamoja na jamaa ama watoto wake bila ya kujinyima.
Bw. Hussein alisema watoto wenye umri wa kuanzia saa moja hadi mika mitano watasafirishwa bure na wanafunzi watatozwa nusu ya nauli ya mtu mzima kwa kila safari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. kazi za kibongo bwana, mkiona kitu kizuri lazima mkakigague na kutoa maelezo mareeefu.kikiwa kibaya nyie haohao mnavutwa pembeni mnanyamazishwa na kukiingiza kimyakimya.
    haya bwana japo kuwa haimaanisha kitu hata kama kwa muonekano ni kizuri kisikaguliwe hapana, sio maana yangu.ninachomaanisha hapa ni inakuwaje vitu vibovu hatupati taarifa zake tunashtukizia kinafanya kazi na ghafla kinatuangamiza ndo ripoti inatoka kuwa ooh kilikuwa kibovu mara hivi mara vile...
    hongera bakhresa, mungu atakuongezea zaidi na zaidi inshaallah,kumbuka mali na watoto ni mtihani.hii ndo raha ya kufanya biashara kwa kutegemea mwongozo wa mungu.
    hongera SSB

    ReplyDelete
  2. Azam wako juu siyo wababaishaji.

    ReplyDelete
  3. tunasubiri ripoti ya wataalamu baada ya ukaguzi.

    ReplyDelete
  4. Tunashukuru Azam Kuleta Ferry sio Meli kama jamaa wanavyodai,kila kinachonunuliwa nje ni kipya?mbona hapo mnakosea.hii ferry ilikuwa inatumika Greece kwenda kwenye visiwa vya Greece na sio mpya kama mnavyodai.
    hata ATC walipoleta Ndege ya kukodi Boeing 737-500 series toka Dubai mkadai ni mpya.siku zote semeni ukweli sio kukisifia chombo kuwa ni kipya na kikija fanya ajali ndio mnaanza kuoakazia kuwa ni mtumba.

    ReplyDelete
  5. Jamani hii ni Ferry au Cruise ship??? Halafu Imetokea Ugiriki? Naomba tuwekewe hiyo ripoti hadharani na sisi tuione manake isije kuwa janga lingine la kitaifa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...