Kamishna kutoka Tume ya Kuratibu na kudhibiti dawa za Kulevya nchini Bw. Christopher Shekiondo akizindua rasmi maonyesho ya sanaa ya Sober House jijini Dar amesema kwa niaba ya tume ya kudhibiti dawa hizo Zanzibar na kwa Serikali kwa ujumla wanatambua mchango wa wadau mbalimbali uliosaidia vijana kuachana na tabia hiyo na kuahidi kushirikiana nao katika kuhakukikisha asilimia kubwa ya vijana wanabadilika kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo sera madhubuti za Serikali na mipango mikakati ikiwemo utekelezaji wa Kampeni za ufahamu wa madhara ya madawa hayo.
Ameongeza kusema kuwa mikakati ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya inakabiliana na changamoto nyingi kutokana na uhaba wa vituo na wataalamu lakini Serikali haijakata tamaa na inaahidi kutimiza lengo hilo katika muda muafaka ikishirikiana na wadau mbalimbali na kuomba wadau wengine wajitokeze.
Mkurugenzi wa Alliance Francaise Tanzania Bw. Sullivan Benetier akitoa hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi katika uzinduzi wa maonyesho ya sanaa ya Sober House Zanzibar ambapo amesema wao wamekuwa wadau wakubwa wa kusaidia mpango wa kuwawezesha vijana kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na kujirudi na kutumia vipaji walivyonavyo kufanikisha maisha yao na kujipatia kipato.
Baada ya kufanikiwa kwa mpango wa kuwawezesha watu wenye ulemavu wa ngozi sasa wamejikita katika kuhakikisha vijana Tanzania wanaachana kabisa na wimbi la matumizi ya dawa za kulevya kwa kuunga mkono shughuli hii ambapo vijana walioonyesha mfano kwa kubadili tabia wanapata fursa ya kuonyesha sanaa zao za kuchora na kuchonga na pia kutokuwa na vipindi vingine vya kutoa ushauri nasaha wa kiakili utakowasaidia kujitambua na kuwafanya kuwa mabalozi watakaoelimusha vijana wenzao kuachana na tabia za matumzi ya dawa hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...