![]() |
| Mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev Kapoor (kulia) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam jinsi vyakula vya asili vinavyoweza kuwavutia watalii kwenda kutembelea nchi mbalimbali na hivyo kukuza utalii wa nchi husika huku Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki akimsikilia kwa makini. Mpishi Kapoor amekuja nchini kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India. |
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev Kapoor (wa pili kulia) mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yao na waandishi wa habari uliohusu umuhimu wa vyakula vya asili katika sekta ya utalii uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Meneja Mkuu wa Hoteli ya Serena Daniel Sambai na kushoto ni Mkurungezi wa Performance Ltd. Tanzania Runjiv Kapur.
Mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev Kapoor (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki leo jijini Dar es Salaam kitabu kinachoonyesha aina mbalimbali za mapishi alizoziandaa katika kipindi cha mapishi kijulikanacho kama Khana Khazana kinachorushwa na Televisheni ya Taifa ya India. Mpishi Kapoor atakuwepo nchini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India. Picha na Anna Nkinda – Maelezo
Ukitaka kumjua Sanjee Kapoor zaidi BOFYA HAPA
Ukitaka kumjua Sanjee Kapoor zaidi BOFYA HAPA





Sanjeev Kapoor Mpishi maarufu Duniani,
ReplyDeleteAndaa angalau ubwabwa wa maana na kutoa Mwaliko sehemu yeyote tuje tujichane hata kwa malipo.
Pana upenzi wa michezo mingi wengine tumeangukia kwenye sahani ya chakula!