Leo ni Jubilei ya miaka 50 ya Hospitali ya Igogwe wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya na Askofu Chengula (pichani chini) ameongoza maandamano ya mamia ya waumini na wadau huko Igogwe na waandamanaji hao wako katika ibada hivi sasa kumshukuru Mungu kwa maendeleo na mafanikio ya hospitali hiyo katika miaka hiyo. Tutaendelea kuwapasha yanyojiri.
Askofu amesema ameshangaa kwa kupendezwa kwa wafanyakazi wa Igogwe kuteua siku ya leo (siku ya Luka mwinjilisti katika kanisa Katoliki,ambae pia alikuwa mponyaji). 
Askofu ametoa rai ya mshikamano katika masuala ya maendeleo. Amerudia ombi la kupatiwa uwanja wa kupanua hospitali kwa kujenga chuo cha wauguzi. Alimuomba Mkuu wa Wilaya(Crispin Meela),aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa (Abbas Kandoro) kufikisha ombi la uwanja kwa mkuu wake. 
Pia vijana kadhaa walipatiwa kipa imara na Askofu Chengula katika Ibada hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...