Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) unapenda kuwataarifu Wateja na  Wananchi wa Dar es Salaam kwa ujumla kuwa taarifa iliyotolewa na Gazeti la kila siku la Mwananchi toleo la siku ya Jumanne Oktoba 02, 2012 kwamba SUMATRA ndiyo kikwazo cha kuanza kwa huduma ya usafiri wa treni jijini Dar es Salaam siyo sahihi.

Katika mchakato wa kutoa  huduma za usafiri wa treni ambayo hapo awali haikuwepo jijini, wadau wa kufanikisha mradi huu  ni taasisi nyingi ambazo zinapaswa kuchangia kuanzishwa kwake. Hivyo basi mchakato huo ni wa lazima na hakuna njia ya mkato . Tunapenda kueleza wazi kuwa  siyo sahihi kusema kuwa TRL imekwama kuanza kutoa huduma ya usafiri wa treni ya  abiria jijini kutokana na SUMATRA kutoidhinisha viwango vya nauli na kutopewa leseni.

Uongozi wa TRL unapenda kutoa rai kwa Waandishi habari na Wahariri wao kabla ya kuchapishwa habari nyeti kama hii inayogusa maslahi ya Wadau wengi na hasa wale wanaongojea kwa hamu huduma hii ianze kujitosheleza  kuwa habari wanayoichapisha ni sahihi na kama inajenga au kubomoa.
  Ukweli ni kwamba TRL hivi sasa inakamilisha mchakato wa kuandaa na  kuwasilisha vigezo ambavyo vinahitajika na SUMATRA ili iweze kufanya tathmini yake na hatimaye kutoa leseni ya huduma ya treni jijini .

Tunarudia Uongozi wa TRL unasikitika kwa usumbufu uliotokana na taarifa hizo zisizo sahihi kwa Wadau wote na hasa kwa  Uongozi wa SUMATRA.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa
Niaba ya  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Mhandisi Kipallo A. Kisamfu
Dar es salaam,
Oktoba 2, 2012






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. TWATAKA VITENDO,Maneno sasa yanachosha!

    ReplyDelete
  2. Mnaaaaaanza sasa Kugongana kweli Bongo Tambarare kweli Msemo wa USITOE AHADI WAKATI WA FURAHA NDIO HUO watu wamesubiri kwa Hamu sasa mvutano jaribuni jamani kujirekebisha WANANCHI WAPATE USAFIRI NA HIZO FENI MSIJE KUZITOA TU. M

    ReplyDelete
  3. Treni hizi ni za kizamani sana. Sijui kwa nini tunaringa nazo. wenzetu walizitumia miaka ya 1960.

    tutafika katua ndogo ndogo.

    ReplyDelete
  4. BS...kumbe hamjajipanga sasa mbona mlituambia mwezi wa kumi? Hizi longo longo zitaisha lini Bongo? Jipangeni kwanza alafu ndio mtuambie lini mtaanza hii kitu.

    ReplyDelete
  5. Suala hili ni la umuhimu mkubwa na pia linawagusa wananchi wengi wa kipato cha kawaida. Sitegemei na wala sipendi siasa katika hali. Taratibu zikamilike haraka ili wananchi waanza kutumia huduma ya treni na kuondokana na adha ya usafiri dar japo kidogo.

    ReplyDelete
  6. Fanyeni utafiti wa kutosha kabla kutoa ahadi zisizo tekelezeka.

    ReplyDelete


  7. hahaha kazi kweli kweli me naona jamani imefika hatua sasa tunatakiwa kumuita raisi ya rwanda aje awe wa Tanzania angalau kwa mwaka 1

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...