Askari Polisi wakichukuwa Maelezo ya Mmoja wa Wahanga wa Mlipuko (wa pili kushoto) uliotokea mapema mchana huu maeneo ya Mikocheni kwa Warioba,Mtaa wa Nyumbu jirani kabisa na Kanisa Katoliki la Mt. Martha.
Kwa mujibu wa Mashuhuda wa tukio hilo,inasemekana kwamba kuna vijana wawili wanaofanya kazi katika nyumba moja inayokaliwa na watu wenye asili ya China,hao waliovalia fulana nyekundu,walitoka na katika nyumba hiyo na lundo la Waya zilizokuwa zimejifungafunga wakielekea kuuza kwa jamaa wa vyuma chakavu waliokuwa wakipita mtaani hapo.
Sasa wakati wanaendelea kuzikunjua waya hizo ambazo zinasadikiwa kuwa ni waya za kopa zitumikazo kama baruti za kulipulia miamba,ghafla zikafanya mlipuko mkubwa na kupelekea wasichana hao wa kazi kudhulika na mlipuko huo.ambapo mpaka sasa mmoja yuko hospitali kwa matibabu na mwingine ndie huyo anaetoa maelezo hapo.
Wakazi wa Eneo la Jirani na nyumba hiyo wakiangalia mabishano baina ya Askari Polisi na Wachina wanaokaa kwenye nyumba hiyo ambao ni Maboss wa wafanyakazi hao walipatwa na mkasa huo.ambapo walikuwa wakiwataka waende nao kituoni kwa ajili ya kutoa maelezo.
Mmoja wa Wahanga wa tukio hilo la Mlipuko akiingia ndani ya nyumba hiyo huku akiwa amejifunika uso baada ya kuumia na mlipuko huo.
Sehemu ya Mabaki ya waya hizo zilizolipuka na kusababisha kizaazaa mtaano hapo.
Wachina siku zote si wastaalamu na wabishi balaa! Serikali ondoeni wachina pelekeni kwao!
ReplyDeletewakiondolewa wachina wewe mlalahoi utafaidika nini? waache ndugu zetu wafaidike kwa kupata vifaa na vitu vya kisasa kwa bei poa kutoka kwa wachina
ReplyDeleteeti serikali peleka wachina kwao ina maana watanzania wote waliokuwa ughaibuni na kule ni kwao?
acha mambo ya kibaguzi kumbuka tupo 2012 maisha ya kubaguana yamepitwa na wakati kenge we.