Timu ya Watanzania wanaoishi katika mji wa Wichita, Kansas, nchini Marekani, imefanikiwa kuichakaza timu ya watani wa jadi  wa Kenya katika mechi iliyochezwa kwenye baridi kali. Ukifanya hesabu za darasa la kwanza za kujumlisha na kutoa, zinaifanya timu ya Watanzania kushinda kwa goli tatu (3) kwa bila (0). Timu ya Timu ya Watanzania inajiandaa kucheza mechi ya marudiano na timu ya Houston Texas, mchezo utakaofanyika Jumamosi ijayo ya tarehe 13, Oktoba, katika jiji la Houston, Texas, nchini humo.
 Mshambuliaji hatari  wa Tanzania Iddi Ligongo akimtoka beki wa timu ya Kenya.
 Hapiti mtu hapa....
Kutoka kushoto walio simama: Juma, Diwani Chehe, Abuusaady Saadiq, Said Saeed, Felix, Deogratias Ngasa, na Idd Ligongo Kutoka kushoto walio chuchumaa Aziz, Ernest, Saleh Kaumbwa, na Denis Rweikiza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ligongo hiyo jezi nyekundu imekupendeza sana kaka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...