Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa akiwa na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu na Mkurugenzi Mkuu wa TRA Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya. wakimsikiliza Mkurungenzi Mtendaji anayeiwakilisha Afrika Bw. Moeketsi Majoro katika mkutano wa IMF nchini Japan- Tokyo
Mhe. Mgimwa na Mkurungenzi Mtedaji anayeiwakilisha Afrika IMF, Bw. Moeketsi Majoro Naibu Katibu Mkuu Bw. S. Likwilile kwenye mkutano wa IMF nchini Tokyo-Japan. Kushoto ni Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu na nyuma ni Bi. Mwanaidi Mtanda Mhasibu Mkuu wa Serikali.
Habari na pPicha na Ingiahedi Mduma na
Scola Malinga, Tokyo- Japan
Waziri
wa Fedha Mhe. William Mgimwa akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa kundi namba moja la kanda ya
Afrika anayewakilisha nchi za Afrika kwenye Shirika la Fedha la
kimataifa (IMF) Bw. Moeketsi Majoro. Hivi karibuni Rais Jakaya Mrisho Kikwete
alimteua Dr. William Mgimwa kuwa Waziri wa Fedha nchini Tanzania ikiwa ni mara
ya kwanza akiwa kama Waziri wa Fedha na
Gavana wa Benki ya Dunia kuhudhuria Mikutano hii ya Benki ya Dunia na shirika
la fedha la kimataifa inayofanyika hapa nchini Tokyo-Japan.
Akiwa katika
Mikutano hiyo, Mhe. Mgimwa amefanikiwa kuonana na Bw. Moeketsi na kufanya mazungumzo
naye mbalimbali mojawapo likiwa ni jinsi gani Tanzania inaweza kufaidika na IMF
na kuweza kuinua uchumi wake kupitia
shirika hilo.
Akizungumza na Bw. Moeketsi, Mhe.Mgimwa alisema kuwa, ” Nina mambo
muhimu kama manne ambayo ukisaidia kufikisha ujumbe huu na kama tutafanikiwa
kupata fedha hizo tutakuwa tumepiga hatua sana katika kuinua uchumi wa nchi
yetu.
"Moja, ni kurekebisha barabara zetu na kuziweka katika viwango vinavyotakiwa, pili ni mfumuko
wa bei, kwakweli mfumuko wa bei umekuwa ukisababishwa na upandaji wa bei za
bidhaa hasa vyakula kama vile mahindi
lakini tumegundua kuwa mchele unapanda
sana hata kuzidi mahindi, tatu ni hii hali ya Tanesco, kwa kweli umeme umekuwa
ni tatizo kwetu pamoja na jitihada zote tunazozifanya na hasa za kutumia
gesi.”alieleza Mgimwa.
Aliendelea kusema kuwa tunahitaji kuimarisha masoko ya ndani na kuwa
na dhamana za kutosha, pamoja na kuwa tumeandaa mipango kamambe ambayo
itatusaidia katika kutekeleza haya lakini bado tunahitaji nguvu kutoka shirika
la fedha la kimataifa”.Naye Bw. Moeketsi
alifurahishwa na uelewa wa Mhe. Mgimwa na kumhaidi kufuatilia kwa karibu, kwani
mambo yote aliyoyaeleza ni ya msingi na kwa sababu yako kwenye mpango mzuri yataweza
kutekelezeka. Mazungumzo ya Mhe. Mgimwa na Bw. Moeketsi yamefungua mianya mipya
na mahusiano ya karibu kati ya na shirika la Fedha la kimataifa na nchi ya Tanzania.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Gavana wa Benki
kuu ya Tanzania Bw. Benno Ndulu,Kamishna wa fedha za nje Bw. Said Magonya,
Bi.Mwanaidi Mtanda ambaye ni Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bw.Beda Shallanda ambaye
ni Kamishna wa sera, Bi. Monica Mwamunyanye ambaye ni Kamishna wa Bajeti, Bw.
Ahmed Rutashobola ambaye ni mwakilishi wa Tanzania huko IMF na baadhi ya
maafisa kutoka Benki kuu na Wizara ya fedha . Aidha Mhe. Mgimwa alimalizia kwa
kueleza kuwa Tanzania imejitahidi sana kupunguza deni la Taifa na vilevile
inafanya jitihada za kuimarisha usimamiaji wa deni hilo kwa kuhamishia jukumu
hilo Wizara ya Fedha ili kuweka usimamizi na udhibiti wa karibu zaidi.
Nchi
za Afrika zimegawanywa katika makundi matatu na Bw. Moeketsi anaziwakilisha
nchi ishirini na moja za Afrika ambazo ziko kwenye kundi la kwanza.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...