Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa mradi wa majaribio wa uwezeshaji wanawake wajawazito na watoto mkoani Mtwara kupata fedha za kununua chakula chenye lishe. Walengwa watakuwa wakipokea fedha kila mwezi kupitia mtandao wa M-PESA. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.
Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan (katikakati)akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa mradi wa majaribio wa uwezeshaji wanawake wajawazito na watoto mkoani Mtwara kupata fedha za kununua chakula chenye lishe. Walengwa watapokea fedha hizo kupitia huduma ya M-pesa. Wengine pichani ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule na Ofisa lishe wa WFP Rosemary Mwaisaka.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...