Joseph Safari Nicetas Mrema
(Julai 26, 1968- Novemba 18, 2011)
Leo tarehe 18/11/2012 umetimiza mwaka mmoja tangu
ulipoitwa na Mwenyezi Mungu. Ingawa haupo nasi kimwili lakini kiroho tupo
pamoja daima na bado tunakukumbuka daima Busara, Hekima, Upendo na Mchango wako
mkubwa katika familia yetu na jamii yote kwa ujumla. Pengo uliloliacha Kaka
yetu mpendwa halitazibika kamwe na hakuna wa kuliziba.
Unakumbukwa sana na
wazazi wako Bw. Na Bibi Nicetas Mrema, Mkeo Sylvia, wanao Theodora, Klein,
Kleist, Bibi yako Jovita, Kaka zako Norbert na Dennis, Dada zako Flora,
Victoria, Ester, Dianna na Lilian, Baba zako wadogo, Perfect, Silvan, Ernest na
Joachim, Wajomba zako, Shangazi zako, Mama wadogo, Mkwe wako, Shemeji zako
pamoja na Ndugu, Jamaa na Marafiki.
Ibada ya kumbukumbu
kwa ajili ya Mpendwa Kaka yetu Joseph Safari Nicetas Mrema itafanyika nyumbani
Mikanjuni Tanga siku ya Jumamosi December 29, 2012.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA
LIHIMIDIWE- AMEN.
Nakukumbuka sana kaka yangu JOSEPH MREMA tangu umetufundisha pale NASACO chekcechea kwa kweli ni pengo kubwa sana kwa familia na kwa sisi pia tuliokufahamu
ReplyDeleteRaha ya milele ummpe eee bwana na mwanga wa milele umwangazie.. Apumzike kwa amani.. AMEN
Mdogo wako
Peter Shirima