Tanzania 50 Plus Campaign ikishirikiana
na wahanga wa saratani na marafiki wa kampeni itatembelea hospitali ya wagonjwa
wa saratani katika hospitali ya Ocean Road. Ili kufanikisha zoezi hilo imeomba watu binafsi na makampuni mbali
mbali na jamii kwa uumla kuchangia sabuni za kufulia, za kuogea, mafuta ya
kujipaka (petroleum jelly), miswaki, dawa za miswaki, ndala, maji ya kunywa,
juice mbalimbali na mtunda.
Katika kuitikia wito huo, Fatma Shabani Msungi, Mheshimiwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kisutu, Kata ya Hananasif,
Wilayani ya Kinondoni, alifika ofisini petu na kukabidhi boksi sita sabuni ya
mbuni. Katika picha ni Bi. Msungi, akiambatana na Kikundi cha akinamama wa
Warembo Forum, akimkabidhi Dr. Emmanuel
Kandusi, Mratibu wa Tanzania 50 Plus Campaign ambaye ndiye anayeratibu ziara
hiyo kuwapa pole na kuwafariji wagonjwa wa saratani. Dr. Kandusi ni muhanga wa
saratani ya tezi dume (prostate cancer).
Tanzania 50 Plus Campaign inamshukuru
sana Mhe. Mwenyekiti kwa ukarimu wake na moyo wa upendo na huruma kwa wale
wenye mahtaji.
Ukiwa na mchango wako wasiliana nasi:
Simu
0754 402033 au barua pepe: ekandusi@yahoo.com,
chrptz@yahoo.com.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...