Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. John Haule kufungua kikao cha Pamoja  cha Maafisa Waandamizi kutoka Tanzania na Malawi kuendelea na majadiliano kuhusu mgogoro wa mpaka kwenye Ziwa Nyasa. Majadiliano hayo yanafanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (mwenye kipaza sauti) akisoma agenda za kikao hicho wakati wa majadiliano. Wengine katika picha ni Mhe. Patrick Tsere (kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Balozi Kasyanju (kulia) na wajumbe wengine kutoka Tanzania.
Wajumbe kutoka Malawi wakimsikiliza Bw. Haule (hayupo pichani) wakati wa majadiliano hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Malawi, Bw. Patrick Kabambe (wa tatu kutoka kushoto) akichangia maoni yake wakati wa majadiliano hayo. Wengine katika picha ni wajumbe aliofuatana nao kutoka Malawi.
Wajumbe kutoka Tanzania wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Malawi (hayupo pichani) wakati wa majadiliano hayo.
Wajumbe wa pande zote mbili wakati wa majadiliano hayo. Picha zote na Rosemary Malale wa Wizara ya Mambo ya Nje

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kwa msimamo wa Malawi sifikiri kama watafikia muafaka, labda roho wa Mungu awashukie Malawi wabadilishe msimamo.

    ReplyDelete
  2. Wasitucheleweshe hawa,

    Nataka watueleze ni nchi gani duniani ambayo kwa ziwa lililopo mpakani inalimiliki lote?

    Unaweza kuwa Msomi au hata ukawa mjuzi sana wa Kiingereza lakini ukawa bado ni mjinga na hujaelimika!

    Hawa jamaa Malawi wanajifanya wanajua sana Kiingereza huku Sheria za Kimataifa zikiwa zimo ktk lugha ya Kiingereza lakini wao wana madai ambayo yamepitwa na wakati.

    Sheria huenda na wakati, ina maana Sheria ya Mkoloni wanayosimamia wao kama hoja ya kulidai Ziwa Nyasa ilishapitwa na wakati na sasa Sheria za Mipaka ya kwenye maji ni za Kimataifa ambapo umbo lolote la maji (ziwa, mto au bahari) la mpakani hugawanywa kwa nchi baina yake.

    Hivi jamani Mjerumani na Mwingereza waliwahi kututawala, hivi inawezekana tukawa bado Sheria walizotuachia tunazitekeleza hadi leo hii?, pana atakaye kubali kuburuzwa Mahakamani kwa Sheria za Mkoloni?

    Waache kuingiza gharama za Vikao na kupoteza muda bureee!

    ReplyDelete
  3. malawi wameshaeleza msimamo wao sasa sijui mazungumzo haya ni ya nini haswa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...