Rais wa Geological Society of America Dr. George H. Davis kutoka Chuo Kikuu cha Arizona akiwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Profesa Sospeter Muhongo kabla ya kumkabidhi tuzo ya HONORARY FELLOW OF THE GEOLOGICAL SOCIETY OF AMERICA (GSA) huko Arizona, Marekani.
Waziri wa Nishati na
Madini, Mhe.Profesa Sospeter Muhongo ametunukiwa tuzo inayojulikana kama Honorary Fellow of
the Geological Society of America (GSA) ambayo hutolewa kwa wanajiolojia
waliobobea kwenye tafiti zinazotambulika kimataifa kwenye mambo ya utafiti wa
miamba na madini (Jiolojia).
Mhe.Profesa Muhongo alitunukiwa tuzo hiyo wakati wa mkutano mwaka
wa Geological Society of America
ulioanza tarehe 3 na kumalizika tarehe 7 Novemba, 2012 katika mji wa
Charlotte, North Carolina Nchini Marekani .Mkutano huo ulienda sambamba na
maonesho mbalimbali ya vifaa vinavyotumika katika kazi za utafiti.
Katika mkutano huo
kulitolewa tuzo 40 za aina tofauti kwa wataalam wa jiolojia ambao
wameweza kutoa michango muhimu katika kuendeleza taaluma ya jiolojia Duniani
kwa manufaa ya binadamu.
Mkutano huo ulihudhuriwa
na washiriki kutoka vyuo vikuu, mashirika mbalimbali yanayojihusisha na
shughuli za kijiolojia, taasisi za jiolojia toka nchi mbalimbali na wanasayansi
zaidi ya 5,000 wenye taaluma ya jiolojia kutoka nchi mbalimbali Duniani.
Tokea GSA ianzishwe mwaka 1888 ni wataalam 44 tu ambao ni wajiolojia na wana anga (astronaut) wameshawahi kutunukiwa tuzo hii. Pia, ilielezwa kuwa Mhe. Waziri amekuwa ni mtu wa kwanza kupokea tuzo hii chini ya Kamati mpya ya Kimataifa inayoongozwa na Prof. Alan Smith kutoka Cabridge University.
Mbali na hii tuzo Mhe. Waziri vile vile alishawahi kutunukiwa tuzo kama hii kutoka Uingereza yaani Honorary Fellow of the Geological Society of London (GSL) ambayo ilianzishwa mwaka 1807. Katika kutambua mchango wa Mhe. Prof. Muhongo Mwaka 2011 Serikali ya Ufaransa ilimtunuku nishani ya Napolion ya Mwaka 1808 kutokana na mchango wake unaotambulika Kimataifa kwenye mambo ya Sayansi.

Imetolewa na,
Fadhili Kilewo
Msemaji
wa wizara

duh jamaa noumer..but unfortunately nobody cares in this country na asipochunga kwenye politics wataishia kum-frustrate bora angebaki huko akaendeleza libeneke la utalaam wake
ReplyDelete