Rais wa Geological Society of America Dr. George H. Davis kutoka Chuo Kikuu cha Arizona akiwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Profesa Sospeter Muhongo kabla ya kumkabidhi tuzo ya  HONORARY FELLOW OF THE GEOLOGICAL SOCIETY OF AMERICA (GSA) huko Arizona, Marekani.

 Waziri wa Nishati na Madini, Mhe.Profesa Sospeter Muhongo ametunukiwa   tuzo inayojulikana kama Honorary Fellow of the Geological Society of America (GSA) ambayo hutolewa kwa wanajiolojia waliobobea kwenye tafiti zinazotambulika kimataifa kwenye mambo ya utafiti wa miamba na madini (Jiolojia).

Mhe.Profesa Muhongo  alitunukiwa tuzo hiyo wakati wa mkutano mwaka wa Geological Society of America ulioanza  tarehe 3 na kumalizika tarehe 7 Novemba, 2012 katika mji wa Charlotte, North Carolina Nchini Marekani .Mkutano huo ulienda sambamba na maonesho mbalimbali ya vifaa vinavyotumika katika kazi za utafiti. 
Katika mkutano huo kulitolewa tuzo 40 za aina tofauti kwa  wataalam wa jiolojia ambao wameweza kutoa michango muhimu katika kuendeleza taaluma ya jiolojia Duniani kwa manufaa ya binadamu. 
Mkutano huo ulihudhuriwa na washiriki kutoka vyuo vikuu, mashirika mbalimbali yanayojihusisha na shughuli za kijiolojia, taasisi za jiolojia toka nchi mbalimbali na wanasayansi zaidi ya 5,000 wenye taaluma ya jiolojia kutoka nchi mbalimbali Duniani.
Tokea GSA ianzishwe mwaka 1888 ni wataalam 44 tu ambao ni wajiolojia na wana anga (astronaut)  wameshawahi kutunukiwa tuzo hii. Pia, ilielezwa   kuwa Mhe. Waziri amekuwa ni mtu wa kwanza kupokea tuzo hii chini ya Kamati mpya ya Kimataifa inayoongozwa na Prof. Alan Smith kutoka Cabridge University.
Mbali na hii tuzo Mhe. Waziri vile vile alishawahi kutunukiwa tuzo kama hii kutoka Uingereza yaani Honorary Fellow of the Geological Society of London (GSL) ambayo ilianzishwa mwaka 1807.  Katika kutambua mchango wa Mhe. Prof. Muhongo Mwaka 2011 Serikali ya Ufaransa ilimtunuku nishani ya Napolion ya Mwaka 1808 kutokana na mchango wake unaotambulika Kimataifa kwenye mambo ya Sayansi.

Imetolewa na,
 Fadhili Kilewo
Msemaji wa wizara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. duh jamaa noumer..but unfortunately nobody cares in this country na asipochunga kwenye politics wataishia kum-frustrate bora angebaki huko akaendeleza libeneke la utalaam wake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...