Bwana harusi Emmanuel Mwangosi akiwa na mkewe Magreth  Mtebe mara tu baada ya kufunga pingu za maisha jana katika kanisa la Agape jakaranda jijini mbeya.Bwana harusi huyu alipata ajali usiku wa kuamkia jumamosi,eneo la Mafiati jijini Mbeya,wakati akiwa na pikipiki yake akielekea kanisani kulikokuwa na mkesha.
Bwana harusi Emmanueli na mpambe wake Frank wakiingia kanisani
Hakika ni furaha hapa bwana harusi anamtambua mkewe kwa kumfunua shela kabla ya ndoa kufungwa
Sasa bwana na bibi harusi wanaingia kanisani tayari kwa ibada ya ndoa
Mchungaji Emmanuel Mwasota toka E.A.G.T toka DSM ndiyo aliyofungisha ndoa hiyo
Hapa bwana harusi akimvisha mkewe pete  huku bibi harusi akiwa katika furaha kubwa na kumshukuru mungu kwa kumuepusha mumewe katika ajali iliyotokea
Hapa wakipata baraka ya ndoa kutoka kwa wachungaji mbalimbali wa kanisa hilo la AGAPE
Sasa tu mwili mmoja kitakachotutenganisha ni kifo tu jina la bwana libarikiwe
Bwana harusi akipokea cheti cha ndoa toka kwa mchungaji Mwasota

Wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kufunga ndoa.Picha zote na Mbeya Yetu Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mungu ni mwema sana.Ni nani anayeweza kututenga na upendo wake, hakuna,Mungu ashukuriwe kijana Emmanuel kwa kukuepusha na kifo.Hutasahau siku hiyo itakupa ushuhuda wa mapenzi ya Mungu daima.Mchumba wako ameonyesha upendo wa dhati kukutunza katika hali hiyo kupiga picha katika hali hiyo,kweli umepata mke mwema.JIna la Bwana na lihimidiwe sana.Mungu awape baraka nyingi katika ndoa yenu.

    ReplyDelete
  2. Neimelipenda tabasamu la Bwana Harusi, kweli duniani wawili wawili

    ReplyDelete
  3. hakika umepata mke mwema.dunia nzima imeshuhudia upendo wake kwake.baraka za mungu ziwatangulie ili huu uwe mfano kwa watu wengine..nimejifunza kitu kutoka kwenu pamoja na kuwa siwafahamu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...