Habari na Picha vyote na
Mdau Atley Kuni wa Mwanza.
"... Mwanzoni nilikuwa sijui kama biashara hii inaweza kunitoa lakini nilipo ianza tu na kujituma Nimeona mafanikio yake...". Ni manene aliyoniambia Kijana Nkwabi ambaye siku zote amekuwa akifanya shughuli zake za picha na kumletea faida kubwa.
Anamuelezea mwandishi huyu kuwa mwanzoni walikuwa wamejikita zaidi kwenye kupiga picha Mitaani, lakini kutokana na adha ambayo wamekuwa wakipata kutoka kwa wateja waliamua kubadili uelekeo na kuanza kupiga picha kwenye Vikao Mbalimbali na hafla zinazo fanyika jijini Mwanza.
Mara ya kwanza alipata shida kidogo kutokana na Aibu lakini aliona hawezi kuendelea kuona aibu wakati ana familia inayo Mtegemea,
"Hakika Ndugu mwandishi huwezi kuamini kuwa kwa siku natengeneza kupata kipato cha kati ya Laki moja na nusu hadi laki mbili", anasema,
Mbali ya hilo kazi ya picha kumuwezesha kwa kipato vilevile imemuwezesha kujenga kujenga Nyumba ya kisasa na anasema anoa wapangaji, aidha kupitia kazi hiyo ya picha ameweza Kununua gari mbili HICE moja na Gari dogo aina ya Mark II.
Kwa upade wake Kamgisha anasema mbali na kupiga picha vilevile kazi hiyo pia imempatia Duka la Vipodozi lililopo eneo la Kilima hewa Stand.
Kijana Nkwabi Mpigapicha Maarufu kwenye Vikao Mbalimbali, akimuonesha Mmoja ya Wajumbe walio hudhuria Mkutano wa Bodi ya Pamba
Mkila Mjue na sisi tunataka hizo Posho tugawane Umasikini
Mzee Hiyo Picha Nitakuuzia Tshs 10,000 tu....
Nikiuza hizi nikimaliza Mkono lazima Uende kinywani. Ndio maneno aliyeo niambia kijana Mwingine aitwaye Kamugisha
hahahaha! hii biashara nzuri si hapa nchini hadi nchi jirani, mkiingia kwenye kikao jamaa wanaanza kazi kabla y kikao, pia picha hizi zinasaidia sana kamati za mazishi kwani miongoni mwa majukumu ya kamati hii ni kupata picha nzuri ya marehemu! hongera kaka posho za vikao tule sote, mie nimetega kuduchi beach hotel,
ReplyDeleteMdau Mbegu.