Staa wa Vichekesho na Filamu Bongo, Said Mohamed Ngamba ‘Mzee Small’ akiwa amelazwa hospitali kutokana na maradhi yanayomsumbua.
KWENU mnaohusika na sanaa ya filamu Bongo. Mnajitambua sina haja ya kuwataja mmojammoja kwa majina, nitamaliza ukurasa bure.
Mimi najua mpo poa, mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku. Binafsi niko poa, naendelea na majukumu yangu ya kila siku ikiwamo hili la kuwaandikia barua.
Barua yangu leo moja kwa moja nailekeza kwa nyinyi wote ambao watu sasa hivi wanawatambua kwa jina la mastaa wa filamu katika soko la Bongo, Bongo Movies.
Kikubwa ni kwamba, natambua mchango mlionao katika kusogeza gurudumu la maendeleo ya nchi. Natambua umuhimu wenu wa kuwatibu watu kisaikolojia kupitia filamu zenu mnazozifanya.
Hongereni kwa hilo.Katika taaluma yangu ya uandishi wa habari, mara kadhaa nimeshuhudia uwezo wenu katika kufanikisha mambo yanayowahusu, iwe ni sherehe au misiba.
Eeeh, kwenye sherehe basi mnalipuka na kushangweka kwelikweli. Kwenye misiba, mnahakikisha mnamsindikiza mtu anayewahusu kwa hadhi anayostahili.
Hoja hapa ni kwamba, hadhi ile ambayo mnajitutumua hadi kwenye misiba, kwa nini tusioneshe kwa mkongwe wa sanaa nchini, Said Ngamba ‘Mzee Small’? Tunashindwa nini? Mbona pesa zipo?
Kwa nini tusimsaidie mzee wetu ambaye tunaimani alikuwa chachu ya vijana wengi kuingia kwenye sanaa?
Mzee wetu anasumbulia na ugonjwa wa kupararazi. Anashindwa kufanya shughuli zake za sanaa ambazo ndiyo chanzo cha pato lake la kila siku.
Binafsi nilisikitishwa na kupongeza kitendo cha Rais wa Shirikisho la Filamu nchini TAFF, Saimon Mwakifwamba kuingilia kati na kuanza kutembeza ‘bakuli’ la michango kwa ajili ya kumsaidia mzee huyo.
Nilisikitika kwani sikuona haja ya yeye kuingilia kati suala hilo ambalo naamini lilikuwa chini ya uwezo wenu, mnaweza bwana! Kikubwa ni kipi haswa? Mbona mna ‘mauwezo’, msinifanyie hivyo bwana.
Kwani kuna tatizo gani tukiweka nukta katika starehe hata kwa siku moja, tusipige kilevi siku hiyo halafu tujichangishe fedha za kumpa sapoti mwenzetu kwenye kipindi hiki ambacho anaumwa?
Hakika hili ni dogo, tukiamua tunaweza tena haliwezi kuharibu bajeti zenu hata kidogo.
Ni yule yule,
Mkweli Daima.
Joseph Shaluwa
Mdau umesomeka nadhani wenyewe watafanyia kazi barua yako.Na sisi tusohusika na sanaa inakuwaje, tunawezaje kumuona mzee wetu japo hata kwa duah.
ReplyDeleteNawakilisha
watanzania ni kama vile kijana ambaye anakaribia kubalehe, au binti ambaye anakaribia avunje ungo, bado anapenda kucheza michezo ya kitoto, lakini wakati huo huo anataka aonekane kama amekua. Tanzania siyo nchi inayofuata ujamaa na kujitegemea, hii siasa ya zamani, bondo sasa ni mabepari na makabaila, wengine wanakula mali za umma bila aibu. katika Mfumo wa sasa kila mti atabeba mzigo wake mwenyewe, kama huna bima ya afya, ndo "arosto" njaa kali, kama ukifukuzwa kazi na huna bima au akiba, wewe jembe ndo linakuita, inasikitisha sana lakini ndiyo ukweli huu, na ukweli unauma.Tumuombee mzee huyu apate nafuu.
ReplyDeleteInasikitisha kwa kweli
ReplyDeleteWala hawana haja ya kuweka sterehe pembeni.Wanaweza kuchanganya sterehe ma msaada. mfano nimeshaona watu wakisaidia watoto yatima kiparty party,watu wana-organise dinner ya kusaidia, wanakutana kwa kiingilio fulani cha kuweza kulipia dinner,kiingilio kikubwa kidogo ili fedha ibaki na zilizobaki zinakwenda kusaidia.
ReplyDeleteKwa hiyo watu wanaweza kukutana hapa kwa kinywaji na party kwa nia ya kuchangisha na kumsaidia mzee. Itakuwa ndege wawili kwa jiwe moja. Kusaidia kwa starehe.
Amelazwa hospitali gani?!
ReplyDeletePitieni kamchango kengine pale magogoni ati, mtu wa wasanii yule
ReplyDeleteKinachokosekana hapa ni Uongozi "Leadership"! Lazima ajitokeze au ajitoe mhanga Msanii yeyote aliyeguswa na tatizo hilo,yeye aanze kupanga "Organise" Utaratibu mzima wa kumsaidia ndugu yetu Mzee Small.Peke yake hatoweza,lazima awe na kikosi kazi cha watu wawili au watatu,watatosha,wasiwe wengi sana.Watambulishe njia zitakazo tumika kuwasilisha michango,kupitia simu za mkononi kama M pesa,nk;iwapo kuna akaunti ya benki ya Mzee Small mwenyewe,au,akaunti maaluma iliyofunguliwa kwa madhumuni hayo,nk.Watu waelezwe ni misaada ya aina gani inayo hitajika "haraka sana,na kwa madhumuni gani",misaada itakayoweza kutolewa polepole kila mchangiaji atakapo pata uwezo wa kufanya hivyo,nk.Ni muhimu watu wakaelezwa "ukubwa wa tatizo lenyewe,aina ya matibabu ambayo lazima Mzee Small ayapate,na Hospitali alikolazwa".Nimetaja mambo ya msingi tu,yapo mengi ya kufanya.Na yanahitajika yafanyike sasa,sio kesho,na sio tusubiri mpaka msiba mwingine utukute,ndipo wasanii waanze vituko vyao vya Mavideo na Makapu ya Mchele nyumbaji kwa Mzee Small!Hebu tubadilike kidogo Watanzania,hususan Vijana wetu.Katika "hili" hakuna atakaye nusurika,sisi sote tuko njiani!Kwa hiyo,natoa rai,kwamba,ili suala hili liweze kufanikiwa na lipate msukumo wa nguvu,ni vyema,Uncle,kwasababu una miliki Blog yako,wewe una nafasi kubwa ya kutufahamisha kila hatua ya kutoa michango na misaada mingine imefikia wapi,na ni mtu tunayekuamini katika hili,"hebu Mungu akupe Ujasiri wa kulisimamia hili",kutoa ni moyo!wala sio utajiri!nawasilisha!mjumbe hauawi jamani!
ReplyDelete