Msanii Costa Siboka 'Mfalme wa muziki wa asili' alipofanya ziara yake wakati wa sherehe za Krismas mjini Moshi. Alifanya utambulisho wa wimbo wake mpya wa WATOTO WANGU ndani ya ukumbi wa kisasa unaokimbiza mji wa Moshi a.k.a Mo-Town unaoitwa ZUMBA LAND. 
Mfalme alifanikiwa kuwapagawisha wakazi wa Moshi kwa kiasi kikubwa ambao kwa kiasi kikubwa waliongozana na watoto wao hata kumfanya ashangiliwe kila dakika. 
Mfalme Siboka ameahidi kuusambaza uhondo huo katika mikoa ya Iringa, Mbeya na Songea kuanzia mwisho wa mwezi Machi mwakani (2013). 
Aidha, Mfalme huyo ameahidi kuimba nyimbo zingine kupitia makabila ya Kihehe, Kinyakyusa, Kingoni na nyingine. Msanii huyu nyota aliyewahi kutwaa taji la Mr Guiness ukanda wa Afrika Mashariki, amekuwa akipata udhamini wa nguvu toka kampuni kubwa ya bia nchini (TBL), Konyagi na Precision Air. 
Unaweza kuwasiliana naye kwa maelezo zaidi: 
0715 499961 na 0787 499961
 Mfgalme Siboka akicheza na watoto  zumba land  siku ya Krismas 2012
Mfalme Siboka na watoto
Mfalme Siboka akiimba wimbo wake mpya wa 'watoto wangu' - Zumba land
Mfalme Siboka akibarizi  mbele ya ndege ya Zumba land
 Mfalme Siboka akitambulishwa kwa mashabiki na mmoja wa wakurugenzi wa Myway Entertainment, Rose Marwa  katika Zumba land mjini Moshi siku ya Krismasi 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...