Mkutano kati ya Ujumbe wa Tanzania na Watanzania waishio Oman ulioanza tarehe 20 umemalizika leo jijini Muscat, Oman. 

Ujumbe wa Tanzania unaoongozwa na Balozi Bertha Semu-Somi, Mkurugenzi wa Masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na unajumuisha wajumbe kutoka Wizara za Mambo ya Nje, Fedha, Viwanda na Biashara, Nishati na Madini, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Miundombinu, Habari na Utamaduni, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu,Afisi ya Rais inayoshughulikia masuala ya Diaspora Zanzibar na Tume ya Mipango Zanzibar.

Aidha, ujumbe umehusisha Taasisi za Serikali za TBC,TIC,TCRA, EPZA, ZIPA, UHAMIAJI, TTB,TANAPA na Dar es Salaam Maritime Institute.

Ujumbe huu umejumuisha pia wajumbe kutoka Sekta Binafsi zikiwemo TPSF, BOA, Azania Bank, CRDB, PBZ, Uhuru One, Zanzibar Issurance Corporation na Zanzibar Chamber of Commerce.

Mkutano wa Diaspora umeitishwa kufuatia maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano uliopita kati ya Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Watanzania waishio Oman ambapo aliwashawishi kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa Tanzania.

Mhe. Rais aliwaahidi kutuma timu ya wataalamu kukutana na Diaspora kuwajulisha juu ya fursa zilizoko nchini na kupokea changamoto zao zinazowakwamisha kuchangia katika uchumi wa Tanzania.

Katika kikao hicho kilichomalizika leo, watanzania waishio Oman wamepata fursa ya kukutanishwa na taasisi za Tanzania na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali ikiwemo kuanzisha mawasiliano yenye lengo la kukuza ushirikiano wa kibiashara. Masuala yaliyojitokeza ni pamoja na haja ya kuanzishwa kwa Chama cha Watanzania waishio Oman.

Oman ni nchi ambayo wananchi wake wengi wana asili ya Tanzania kutokana na uhusiano wa kihistoria baina ya nchi hizi mbili. Inakadiriwa kuwa familia 780 za Watanzania wanaishi nchini Oman na kuendesha shughuli zao katika sekta binafsi na Serikali.

Mhe. Balozi Bertha Semu Somi, Mkurugenzi wa Masuala ya Diaspora akimfafanulia jambo Prof. Msafiri Mbaga ambaye ni Mtanzania anayeishi na kufundisha nchini Oman.
Sehemu ya Watanzania waishio Oman wakishiriki ufunguzi wa Mkutano.
Bw. Twisa Mwambona, Meneja wa Azania Bank akizungumza na Meneja wa Masuala ya Credit na Risk wa Bank of Oman.
Kamishna wa Hazina(Kulia) akitoa maelezo ya ufafanuzi wa Diaspora kuhusu Sheria za Fedha na Kodi nchini Tanzania. Katikati ni wadau kutoka Wizara ya Uchukuzi.
Bi. Josephine Kimarowa Menejimenti ya Utumishi wa Umma (katikati) na Bw. Joseph Haule wa Wakala wa Ajira(Kulia) wakizungumza na mdau aliyetaka kufahamu kuhusu fursa za huduma za Ajira na Utafiti (Consultancy) nchini Tanzania.
Bw. Hassan Hafidh kutoka Afisi ya Rais-Diaspora Zanzibar akizungumza na wadau wa Diapsora juu ya mipango ya Serikali ya Mapinduzi wa Zanzibar kwa Watanzania wenye asili ya Zanzibar waishio nje.
Bi. Patricia Nguma kutoka BOA Bank(kulia) akijadiliana na Mdau wa Diaspora kuhusu mikopo ya nyumb ya BOA.
Bw. Boniface Ngowi wa Wizara ya Viwanda na Biashara akitoa maelezo kwa Watanzania waishio Oman kuhusu Sera za Biashara nchini Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ni kitu kizuri sana kujaribu kuwatumia wenzetu wa diaspora kuleta maendeleo ya nchi. Nchi za wenzetu walishafanya hivyo no millions of dollars zinaenda nchini kwao kutoka diaspora. Ispokuwa,just a word of caution,pamoja na nia njema ya serikali kuwavuta wenzetu wa dgiaspora kuwekeza nyumbani,ule urasimu,unnecesery red carpet blockages lazima ziondoke. Kurefusha mambo ili kutengeneza mzingira ya rushwa iondoke. Usumbufukwa mfano,mtu akitaka kufungua kampuni BRELA uondoke,kufungua kampuni while u have all the docs inachukua two weeks or more,watendaji pale are unfriendly,hawako tayari kujituma kumsaidia mteja,mtu akiulizwa swali anaona usumbufu......nk,haya yoge yaende sambamba na jitihada zinazofanywa na serkali kuwavuta wenzetu wa diaspora. Tusiwaite halafu wakajutia maamuzi yao ya kuja nyumbani kuwekeza. Asante Ankal.

    ReplyDelete
  2. Wapinga Muungano Zanzibar mmeona hiyo?

    Angalieni waliopo Uarabuni tena wanaokula tende kwa maziwa wanaona thamani ya Muungano, waneupenda Muungano na wapo tayari kuusimamia Muungano !

    Angalieni picha ya chini kabisa hadi raha!!!, RAIA WAUNGWANA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKIWA UGENINI OMANI WAMEWAPOKEA KWA MOYO WA DHATI KABISA MAAFISA WA SERIKALI KUTOKA NYUMBANI TANZANIA WANAWASIKILIZA KWA MAKINI KABISA, NA KUONYESHA YA KUWA WAPO TAYARI KUIJENGA NCHI HATA KAMA WAPO HUKO UGENINI!!!

    SASA NINYI MLIOPO HAPO KIEMBE SAMAKI ZANZIBAR HATA RASI-NUNGWI PENYEWE HAMJAPITA MNAKATAA MUUNGANO?

    TUWAELEWE VIPI?

    ReplyDelete
  3. Hongera serikali.

    Hii ni ziara yenye faida kubwa sana kwa nchi!

    ReplyDelete
  4. Mnaona ?????

    Masheikh wa Oman ndio kwanza wanaunga Mkono MUUNGANO na Kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

    Je, ninyi Masheikh wa Madevu madevu wa Uamsho mko msimami gani kuupinga Muungano?

    ReplyDelete
  5. Uamsho na Wapinga Muungano mmeona hii!!!,


    Harakati zenu zinatokea wapi, zinatokea Malawi?,

    Mmeona Masheikh wenye akili waliopo huko Omani wanashiriki na kuunga mkono Muungano hapo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...