WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amepiga marufuku na kuagiza kuondolewa vizuizi vyote vilivyoanzishwa na Halmashauri kwenye stendi za barabara kubwa kwa ajili ya kukusanya ushuru kwani vinaleta usumbufu kwa abiria.

Kauli hiyo ilitolewa na waziri huyo jijini Dar es Salaam, wakati alipofanya ya ziara ya kushtukiza kwenye Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi majira ya saa 11:30 alfajiri, ili kujionea utendaji kazi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), na Kikosi cha Usalama Barabarni (Trafic), haswa katika udhibiti wa nauli holela katika kipindi hiki cha sikukuu ya Chrismas na mwaka mpya.

Alisema uwamuzi wake huo unatokana na kubaini kuwa Halmashauri hizo, zimekuwa zikiwalazimisha madereva kuingiza magari (Mabasi), kwenye vituo hivyo ambavyo siyo rasmi kwa lengo la kujikusanyia ushuru.

Amevitaja vituo hivyo vilivyolalamikiwa kwa usumbufu huo, kuwa ni pamoja na Mafinga, Kibaigwa, Nzega, Kibaha na vingine.

“Madereva wamekuwa wakilazimishwa kuingia katika stendi hizi hata kama hawana abiria wakushuka amakupakia, kitendo ambacho kinawapotezea abiria muda wao wakufika kule wanakokwenda bila sababu za msingi”alisema Dk Mwakyembe.

Alisema utaratibu huo haukubaliki, endapo ukiachwa uendelee hivyo iko siku watazuka watu watafikia hatua ya kuanzisha vizuizi kama hivyo majumbani mwao lengo likiwa ni kuibia wananchi.

Dk Mwakyembe amezitaka Halmashauri hizo kuacha utaratibu huo na baadala yake watafute vyanzo vingine vya ukusanyaji mapato.

Katika hatua nyingine Dk Mwakyembe amewaonya baadhi polisi wa kikosi cha usalama barabarani kutokana na mtindo wao wakusimamisha magari kwa kushtukiza wakitokea vichakani.

Alisema malalamiko hayo ameyesikia siku nyingi hivyo ameahidi kuwa atayafanyia kazi, ambapo aliwatahadharisha askari wenye tabia kama hizo, watambuwe muda wao sasa unahesabika.

Akizungumzia hali ya usafiri katika kipindi hiki cha sikukuu hizo mbili, Alisema hali aliyoikuta Kituoni hapo inaridhisha kwakuwa abiria wote kwenye mabasi walikuwa wamepata tiketi kwa bei elekezi ya Sumatra.

Dk. Mwakyembe alitoa wito kwa abiria wote kuwa wahakikishe wanatoa ushirikiano kwenye vyombo vinavyohusika pindi watakapotozwa nauli kinyume na ile ya kawaida.

“Msikubali kulipishwa zaidi toeni taarifa haraka, hata katika nauli za mizigo msikubali kulipia mzigo wa kilo 20 atakaekubali yote hayo mtambue amejitakia mwenyewe na asilaumiwe mtu”alisema.

Naye Kaimu Mkurugezi Udhibiti Usafiri wa Barabarani (Sumatra), Leo Ngowi, alisema katika operesheni inayoendelea ya kuyakamata magari yanapandisha nauli holela jana, walifanikiwa kulikamata basi la Kampuni ya KVC lenye usajili namba T709AAT.
Alisema gari hilo lilikwenda kinyume kwa kuwatoza nauli ya sh 35,000 baadala y ash 25,000 abiria waliokuwa wakisafiri kwenda Arusha.

Aidha, Sumatra imetoa leseni za muda kwa wamiliki magagri ambayo yamekidhi viwango vilivyohitajika na mamlaka hiyo, yenye uwezo wa kuchukua abiria 30 kwa lengo la kusaidia kusafirisha abiria wanaofika kwa wingi kituoni hapo ambapo mikoa inayoongoza kwa abiria ni Kilimanjoro, Arusha na Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Huo ulikuwa wizi wa wazi kabisa. Nakumbuka tulilazimishwa kuingia kituoni pale Segera, wakati hakukuwa na abiria wa kushusha, na kituoni hakukuwa na abiria yeyote, ambaye labda alihitaji usafiri! Hongera Mwakyembe, tunataka watendaji kama wewe, sio wapiga porojo majukwaani na magazetini kama UDASA!

    ReplyDelete
  2. Mzee Mwakyembe hana mpinzani Tanzania.kama anaweza kusport matatizo ya watanzania kama hayo tofautiuti na wafalme wa wizara nyingine.inaskitisha waziri aliyepewa mamlaka yote na wananchi anapobaki kulalamika akiwa ofisini na sijui sisi wananchi tufanyeje.waziri anabaki ofisini akilalamika kwenye kochi la kodi zetu.haina budi mawaziri wote kuiga kutoka kwa mh Mwakyembe kwani anaenda kwenye kiini cha matatizizo na si kulalamika ofisini.

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Dk Mwakyembe. Tumekuona mara zote ulipotukimbilia wanyonge katika matatizo yetu hususan ya usafiri. Tafadhali fika na mikoani pia kuna issue nyingi kama za hapo Dar-Watendaji huku bado wamelala usingizi na unapojaribu kuwaamsha watadai rushwa na visingizio lukuki-Wizi mtupu!! Heri ya Xmas na Mwaka mpya Dk. Keep it up 2013!!

    ReplyDelete
  4. Hongera Sumatra Tumeona mlivyowadhibiti wenye magari na lakini zaidi wenye uchu na uroho wa utajiri kupitia ulanguzi na wizi wa tiketi kwa abiria na mizigo yao. Kazeni buti na isiwe wakati huu wa sikukuu tu! Iwe zoezi endelevu wakome kutuibia Tumechoshwa Mbarikiwe sana Herini ya Xmas na mwaka mpya 2013

    ReplyDelete
  5. Hongera sana Mheshimiwa.
    Kwa upande wa mizigo sisi abiria wa Kusini tunanyanyaswa sana na wenye mabasi. Kimzigo kidogo hata kilo kumi hakifiki unatakiwa ukilipie.

    Tafadhali tunaomba ufanye msako wa kushtukiza kule Mbagala wakati yanaondoka uone jinsi watu wanavyolalamika.

    ReplyDelete
  6. Hongera dr kwa juhudi zako. Watanzania tupo pamoja na wewe, tutakupigania siku zote kwa sala na maombi. Jamani fanyeni kazi hatujawachagua kutuuzia sura zenu, na wale mashakubembe muache kumwanadama, dr wetu. Mushindwe na mulegee wote mnaompiga vita dr mwaki

    ReplyDelete
  7. Chriss KinaboDecember 24, 2012

    Kusemna kweli SUMATRA nimewafagilia sana sana safari hii, mmefanya kazi kubwa sana sana pamoja na uchache wenu lkn mmeonyesha mnaweza. naweza kuwahakikishia kuwa ndani ya mabsi tuliyokuwa tunasafiri nayo hawa jamaa wa Ubungo wanawaogopa SUMATRA kuliko jeshi la Polisi.
    Na walikuwa wanatueleza eti tukiulizwa na SUMATRA tumelipa ngapi tuseme 20000!
    Asante Ndugu Shayo na timu yako kwani mie nilirudishiwa 10,000 yangu japo njiani walinisakama sana.

    ReplyDelete
  8. Mheshimiwa waziri angalia mambo mengine, sisi tafiki tulionunua tochi wenyewe tutarudishaje pesa zetu kama hatutojificha?

    ReplyDelete
  9. Dr. Mwakyembe,

    Chukua ile NYUNDO YA C.C.M uitumie kupiga na kuvunja vunja wizi na uovu wooote!

    Kama utaona pana vizuizi CHUKUA PIA JEMBE LA C.C.M LENYE MAKALI CHAPA MAMBA ukwatue mpaka mizizi ikilegea na kukatika halafu SHUSHA NYUNDO KWA NGUVU MPAKA VISIKI VYA WIZI VING'OKE !!!

    TANZANIA BILA WIZI INAWEZEKANA!

    ReplyDelete
  10. Mhe. mwakyembe wakati Ukiitumia vizuri Nyundo nzito yenye mpini wa Chuma ya Chama cha Mapinduzi kugongea sehemu zenye uozo, tunakukabidhi na Gunia la MISUMARI ili ugongelee sehemu zote zenye mianya na penyo za wizi na Ufisadi !!!

    Atakaye weka mikono yake itakuwa imekula kwake atakwenda Hospitali kuchomolewa misumari na kudungwa sindano za tetenasi yeye mwenyewe!

    ReplyDelete
  11. Sasa tumepata wakutuongoza katika hili. Wananchi wote tunapaswa kuunga mkono jitihada zote zinazofanywa na viongozi wazalendo kama Dk. Mwakyembe, watanzania tumechoshwa na maneno na ahadi zisizotekelezeka. Hongera Dk. Mwakyembe chapakazi tuko pamoja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...