Enzi hizo bila ngoma ya Michael Jackson (RiP) ya 'Don't stop till you get enough' disko lilikuwa halinogi...hasa kwa kuwa MJ alikuwa bado Mmatumbi halisi. Wenye data ya enzi hii kazi kwenu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Labda nimsaidie uncle kwa hili, enzi hizo ilikuwa ni yale ma'LP', yaani marekodi yale makubwa, na tulikuwa tunasubiri kwa hamu jamaa kutoka Ulaya walete hizo rekodi ili na sisi turekodi kwenye kaseti (sijui hakukuwa na copyright enzi hizo?).

    Hii ni rekodi ya kwanza ya MJ kama solo artist baada ya kutengana na kaka zake (Jackson five ambao nao walikuwa moto wa kuotea mbali).

    Na hii rekodi mtaani kwetu ilikuwa inajulikana kwa jina 'Kiboribo' - maana ile don't stop till you get enough watoto wa mtaani walikuwa hawaipati ile lugha.

    ReplyDelete
  2. AHSANTE KWA 2X2 !

    Balozi Ankali Michuzi,

    Ninashukuru sana na kufarijika na usikivu wako!

    Ni vile umeweza kufahamu kuwa ni MUHIMU KUZINGATIA ZILE ZA KIPINDI CHETU KILEEE WEWE NA MIMI , NA PIA KUWASIKILIZA HAWA MADOGO WA KIZAZI KIPYA KWA KUWAPA KETE ZAO !

    HUU NI MPANGO MZURI WA KUDONDOSHA MBILI MBILI (2X2)

    HIVYO NGOMA DROO (ZAMANI NA SASA) HAKUNA WA KULALAMIKA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...