London Interbank Offered Rate (LIBOR) ni makadirio ya kiwango cha riba kinachotumika wakati benki zinapokopeshana pesa. Kiwango hicho cha riba kinatumiwa na mabenki yanapokopeshana kwa kulipa mikopo ya muda mfupi na muda mrefu (siku moja, mwezi hadi mwaka) Kiwango hicho kinawekwa na British Bankers’ Association (BBA) kila siku saa tano asubuhi kwa time za Uingereza.

Tatizo la riba ya LIBOR na ambalo lilipelekea mwenyekiti wa Barclays, Marcus na (Chief executive) wa Barclays Bob Diamond nchini Uingereza kujiuzulu Jumatatu ya tarehehe 2/07/2012, limechukua mkondo mwengine. Ofisi inayoshughulika na maswala ya ufisadi mkubwa inayojulikana kama The Serious Fraud Office (SFO) imewakamata watu watatu kama hatua ya uchunguzi kwa sababu ya kuhusika kwao na ufisadi huo. Ripoti hiyo ilieleza kwamba watu watatu wote wakiwa raia wa Uingereza wenye umri wa miaka 33, 41 na 47 wamekamatwa na wamefikishwa kituo cha polisi ktk jiji la London kwa ajili ya mahojiano kwa madai kwamba walidanganya wakati wa kutoa makadirio ya kiwango cha riba.

LIBOR inaathiri makadirio ya zaidi ya pound 350 trillion ya matumizi ya pesa ulimwengu mzima, na kiwango kinachotaja na LIBOR kina ushawishi mkubwa duniani ktk matumizi mengi ya kifedha ikiwemo mikopo. Taasisi karibu 16 za kiuchumi ulimwenguni zinachunguzwa kuhusiana na madai hayo. Kwa upande mwengine Royal Bank of Scotland inategemewa kutangaza jinsi itakavyolimaliza tatizo hilo wakati benk kubwa ya nchini Swiss, Union Bank of Switzerland (UBS) inategemewa kufikia makubaliano ya kumaliza tatizo hilo.

Kuhusu swala la LIBOR na mengineyo yanayohusu benki zinazofuata sheria ya kiislam, wasiliana na  http://ijuebankyakiislam.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Royal Bank of Scotland na UBS (Union Bank of Swiss) wasipoteze muda kuhangaika bureee,

    Suluhisho la tatizo hilo jibu lake ni kuhamia kwenye COMPLIANCE AND DEEDS BANKING (Islamic Banking) badala ya kuendelea na Mfumo wa Kibenki wa Makadirio ambao ni kama RAMLI YA KWA MGANGA WA KIENYEJI kitu ambacho inaweza kuwa ni sawasawa au la.

    Mfano kwa wale wenye Taaluma ya Mahesabu pana kitu kinaitwa 'exageration' ni kama kutia chumvi au kuvumisha kitu ambacho hakina uhakika panatakiwa Mfumo ambao unatoa uhalisia na uhakika badala ya Mfumo wa Makadirio kama wa hao Waheshimiwa LIBOR.

    Jibu ka tatizo ni hao LIBOR kufuta Msamiati wa Riba (Interest) katika Computer zao na kuweka Msamiati mpya wa suluhisho la tatizo wa COMPLIANCE/DEEDS!

    ReplyDelete
  2. Duhhh ama kweli Dunia imekuwa chini ya udhalimu kwa miaka mingi sana!.

    Sasa ina maana hiyo Net Present Value (NPV) yaani [{NPV=In-Io}, where In>Io] tofauti kati ya kiwango halisi cha Riba na ile ya makadirio kimekuwa kikiwanufaisha hawa watu sana!

    ReplyDelete
  3. Kwa kuwa Fedha ni Non-homogeneous goods (bidhaa), huku Rate of Interest is determined by (i)Liquidity preference and (ii)Money supply (Mahitaji na upatikanaji Sokoni) at the Financial Market.

    Hivi kumekuwa na sababu gani hawa LIBOR wasiache kuikadiria Riba ili iweze ikaamuliwa na Market Forces yaani Demand and Supply?

    ReplyDelete

  4. Inadhaniwa kwamba ushauri mzuri ni kutumia kiwango cha faida au hasara kwa kuangalia soko la biashara kama inavyofanya na the Islamic Interbank Benchmark Rate (IIBR) iliyoanzishwa mwaka 2001 kwa kuepuka matatizo kama hayo. Hatua nyingine ni ile ya kuepuka mazingira yasiyoeleweka ktk biashara kama vile kamari (speculation) na hadaa (gharar), na kuzuia biashara ambazo sio halali kisheria. Moja ktk kuepuka hasara kama hizo benki zinazofuata sheria za kiislam zinatumia utaratibu wa kwamba faida ya mtaji ktk uchumi wa kiIslam inategemea jinsi gani mjasirimali atakua tayari kukubali hasara inayotokana na biashara na sio kutegemea riba. Upande mwingine ni ule unaohusiana na kuuza deni pamoja na kutaka uhakika (guarantee) ya faida, hilo haliruhusiwi ktk sheria ya kiIslam na badala yake mifumo mingine ya kibiashara inaweza kutumika kama vile Mudarabah na musharakah.

    ReplyDelete
  5. Infact,these same countries enjoying the flexibility of Islamic Interbank Benchmark Rate (IIBR),are reportedly,The Most Indusrialised Countries in the World,according to the Islamic World Bank Factfile!

    ReplyDelete
  6. wanadamu mshaelezwa kuwa riba ni dhambi sasa baada ya kuwa tamu inakuwa chungu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...