Meneja Mwandamizi Idara ya Utendaji wa Benki ya NBC, Salim Rupia (kulia) akikabidhi msaada vyakula na vitu vingine vilivyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo kwa Katibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWAMA, Ally Saidi kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Sikukuu za Christmas na mwaka mpya. Wafanyakazi hao walichanga zaidi ya shs milioni 3 kwa ajili ya vitu hivyo na sehemu ya pesa itatumika kulipia ada za shule kwa baadhi ya watoto mwakani. Wengine ni baadhi ya wafanyakazi hao na watoto wa CHAKUWAMA.
Meneja Huduma kwa Wafanyakazi wa NBC, Suzyo Gwege-Nyirenda (kulia) akikabidhi msaada vyakula na vitu vingine kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha CHAKUWAMA, Sinza jijini Dar es Salaam vilivyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Sikukuu za Christmas na mwaka mpya. Wafanyakazi hao walichanga zaidi ya shs milioni 3 kwa ajili ya vitu hivyo na sehemu ya pesa itatumika kulipia ada za shule kwa baadhi ya watoto mwakani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...