--
Mabondia wa Tanzania jana waling'ara katika mapambano yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala Zakhem. Bondia maarufu nchini, Mada Maugo alimchapa Yiga Juma kutoka Uganda raundi ya kwanza kwa ‘Knock Out’. Katika hali iliyoonesha kuwa siku ya vichapo kwa wageni, pambano lingine ambalo bondia Mbwana Matumla alipambana na bondia kutoka Kenya, David Charanga lililokuwa la raundi nane, Matumla aliibuka kidedea katika raundi zote nane na kumfanya aibuke na ushindi wa kishindo.
(PICHA NA ISSA MNALLY NA RICHARD BUKOS / GPL)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...